Vyanzo vya moto mabwenini

Vyanzo vya moto mabwenini

KAKA NASOKI

Senior Member
Joined
May 25, 2016
Posts
191
Reaction score
212
Nimeipata mahali si vibaya ku-share

Poleni kwa majanga ya moto mashuleni. Hivi punde jamaa alimfanyia interview mwanafunzi aliyemaliza form six, akasema alimwambia mashule yanaungua kwasababu huwa wana simu na huwa zinafichwa darini, wakitaka kuchaji wanakwangua waya wa umeme wanategeshea chaji zao, na huwa wanafanya usiku wakati wa preparation (prep )ya jioni, kwahiyo mabweni huungua kuanzia darini sababu ya kukwanguliwa nyaya za umeme. Hivyo moto ukizuka inaonekana ni hitilafu ya umeme.

Aliulizwa kama walimu wanalijua hilo akasema hadi leo hawjui kama wao ndio wanasababisha.

Jamani tuwajulishe Walimu na wenye shule wawe wanafanya ukaguzi kwenye dari za mabweni mara kwa mara. Na wale wanaokagua chanzo cha moto wawe wanahoji vijana kwa kina wapate taarifa kamili, kuepuka ku conclude wiring za mashule ni mbovu.

Chanzo kingine ni kutumia heater za kienyeji kuchemshia maji ya chai, zilizotengenezwa kwa spring za vitanda vya chuma, ikitokea zile spring mbili zinazo ning'inizwa kwenye jagi la maji zikigusana hakuna kingine ni moto.
 
Kuna shule iliungua japo haikuwa na umeme, wanatumia taa za sola. Hili limekaaje mkuu. Maana hili la kuchaji simu litakuwa chanzo iwapo tu, shule ina umeme.
 
Umepewa sababu ya kawaida sana na wewe umeingia kingi kuamini hiko ndio chanzo kikuu?

Rudi ukamuulize kwa nini shule nyingi zilizoungua mwaka huu ni za kiislam tuu?

Halafu hayo mambo ya kuchaji kwa hiyo style ni ya enzi na enzi na yanajulikana, hata sisi wa miaka hiyo simu zinaingia tumefanya sana, shoti inayosababishwa na hiyo style ya kuchaji huwa ni ndogondogo ambazo mara nyingi huwa zinafanya main switch ijizime then mnaweka mambo sawa mnaenda kuiwasha maisha yanaendelea.
Unforgetable
 
Ubaya kuna wazazi ambao wanawapa watoto hizo sim na kuwaelekeza jinsi ya kuzitumia kwa vificho wawapo mashuleni. Nimelisikia hili kwa mtoto wa 12years anayesoma boarding

Nilichojiuliza ni kwamba
Hivi mzazi anayempa mtoto sim aende nayo shuleni kinyume cha sheria anakua amempeleka mtoto wake shule kusoma?
au ndio anayewezesha mawasliano ya kuhujumu hizi shule?
Huyu mzazi ni mawasliano gani anafanya na huyu mtoto na kwa faida gani?

Shule ziongeze ujuzi kwenye kudeal na hawa vijana wetu. Kuwe na sheria Kali sana kwa kosa Hilo na wazazi tusiache kutoa ushirikiano kwa walimu ambao ndio walezi.
 
Kuna shule iliungua japo haikuwa na umeme, wanatumia taa za sola. Hili limekaaje mkuu. Maana hili la kuchaji simu litakuwa chanzo iwapo tu, shule ina umeme.
Solar ni umeme ndio mana inwasha TV unless haina Inverter, kwani sola kuna mpaka za kuendesha pump na kuchemshia maji ya kuoga hasa mbugani kwenye camps zilizoko Serengeti, Tarangire, Selous nk.
 
Naelewa. Lakini unazifahamu taa za solar nilizozungumzia? Ni zile taa zenye sehemu ya panel mojakwamoja. Unakuta vimetundikwa mabwenini muda wa jioni.
 
Kwahiyo unasema wanachoma moto Au? Na ile miaka shule za Kikristo zilipokuwa zinaungua zilichomwa? Kuna watu na watu jamani kwa hiyo watu wa ukoo mmoja wakifa mfululizo kuna mkono wa mtu?
 
Nimeipata mahali si vibaya ku-share

Poleni kwa majanga ya moto mashuleni. Hivi punde jamaa alimfanyia interview mwanafunzi aliyemaliza form six, akasema alimwambia mashule yanaungua kwasababu huwa wana simu na huwa zinafichwa darini, wakitaka kuchaji wanakwangua waya wa umeme wanategeshea chaji zao, na huwa wanafanya usiku wakati wa preparation (prep )ya jioni, kwahiyo mabweni huungua kuanzia darini sababu ya kukwanguliwa nyaya za umeme. Hivyo moto ukizuka inaonekana ni hitilafu ya umeme.

Aliulizwa kama walimu wanalijua hilo akasema hadi leo hawjui kama wao ndio wanasababisha.

Jamani tuwajulishe Walimu na wenye shule wawe wanafanya ukaguzi kwenye dari za mabweni mara kwa mara. Na wale wanaokagua chanzo cha moto wawe wanahoji vijana kwa kina wapate taarifa kamili, kuepuka ku conclude wiring za mashule ni mbovu.

Chanzo kingine ni kutumia heater za kienyeji kuchemshia maji ya chai, zilizotengenezwa kwa spring za vitanda vya chuma, ikitokea zile spring mbili zinazo ning'inizwa kwenye jagi la maji zikigusana hakuna kingine ni moto.
Mbona ni shule za kiislam tu?
 
Kuna shule iliungua japo haikuwa na umeme, wanatumia taa za sola. Hili limekaaje mkuu. Maana hili la kuchaji simu litakuwa chanzo iwapo tu, shule ina umeme.
Hapana, wanatumia taa za umeme wa solar
 
Hiyo ya kuchaji cm darini hata mimi niliifanya sana. Ukikosea kuconnect nyaya umeme unajikata bweni zima
 
Ubaya kuna wazazi ambao wanawapa watoto hizo sim na kuwaelekeza jinsi ya kuzitumia kwa vificho wawapo mashuleni. Nimelisikia hili kwa mtoto wa 12years anayesoma boarding

Nilichojiuliza ni kwamba
Hivi mzazi anayempa mtoto sim aende nayo shuleni kinyume cha sheria anakua amempeleka mtoto wake shule kusoma?
au ndio anayewezesha mawasliano ya kuhujumu hizi shule?
Huyu mzazi ni mawasliano gani anafanya na huyu mtoto na kwa faida gani?

Shule ziongeze ujuzi kwenye kudeal na hawa vijana wetu. Kuwe na sheria Kali sana kwa kosa Hilo na wazazi tusiache kutoa ushirikiano kwa walimu ambao ndio walezi.
mzazi mbwiga huyo, anahisi eti ndo anampenda mtoto sana akifanya hivyo
 
Back
Top Bottom