Vyanzo vya ajali ni Serikali yenyewe kupitia vyombo vyake

concordile 101

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
1,413
1,763
Kiharaharaka kila ajali inapotokea tumekuwa wepesi kuwatupia lawama madereva au wamiliki wa vyombo vya usafiri bila kuangalia upande wa pili wa shilingi.

Katika mihangaiko yangu nishakutana na ajali kama nne kubwa ikiwa air msae mwaka 1996. Kipindi chote na mimi niliamini vyanzo ni madereva mpaka na mimi nilipohitimu kununua kijiusafiri.

Kwa ujumla ukilinganisha na nchi za wenzetu kwetu hata kama tutaweka tochi kila baada ya mita ishirin ajali zitazidi kuwepo.

Sababu ya ajali ni kama ifuatavyo:-

1) Stress kwa madereva.
90% ya madereva wa mabasi hawalipwi mishahara bali posho. Letsay unakuta dereva anapewa siti mbili za nyuma kama ndo mshahara per day sasa siku gari ikiondoka empty wakiingia barabarani ndo balaa matrafiki ukiona umesimamishwa hasa mida ya asubuhi kabla hela ya chai haijapatikana hutoki.

Hivi inakuwaje kuwe na fine eti kwa kukosa sticker tu ya nenda usalama. Umenipiga fine letsay nikalipa 60000 na ndo ilikuwa posho yangu huko barabarani nitakuwa normal? Upande wa pili mke anahitaji hela ya mtoto anaumwa.

2) Upangaji nauli badala ya kuacha nauli ijipange kulingana na soko.hii imepelekee matajiri kujaribu kuminimize cost kwa njia zozote sabab nauli inayopangwa haiwezi kufidia uwekezaji kwa muda muafaka. Njia iliyobaki ni kufanya manunuzi ya mabasi ya bei rahisi ambayo nchi kama south afrika hayaruhusiwi kukanyaga. More than hata utakuwa tayari kuleta vitu vizuri bado sheria sio rafiki. Mfano wakati wenzetu zambia waeruhusiwa kuwa na double deckers kwetu urefu huo hauruhusiwi. Pia bus haziruhusiwi kuzidi mita 14. Kati ya mabus ambayo ni salama sana ni mabus ya rear engine lakin kulingana na sheria zetu za mizan ambapo gari halitakiwi zidi 18ton, ni nan ataweza leta bus hizo kwa wingi. Kipindi cha sumry ilikuwa kila mzan watu wahame nyuma. Ukifuatilia magari mengi pale ubungo ni mabovu ukizama chini ya uvungu huwez amin. Tumebaki kukimbilia vya china ambavyo wakati wa mvua vinateleza mitaroni tu.
3) barabara ni mbovu sana. Hiki ndo chanzo kikubwa sana mfano mlandiz- chalinze ila ajari ikitokea utasikia dereva. Njoo mtwara lindi,morogoro dodoma zote hizo sio barabara za kulaumu. Zaidi ya hapo si ajabu ukapita sehem hakuna hat kibao au unakuta bump jeusi halina hata mistari ya kuonesha kuna bumb. Kuna sehem vibao vimefichwa makusudi tu ili tupigwe fine.kwa wenzet huko bus lina cruise mpk speed 140 na hata husikia kukurukakara.
TUNATATUAJE
badala ya viongoz wetu kukaa maofisin na kufanya maamuzi waje kwa wadau tushirikiane jinsi ya kutatua tatzo ishu sio upande wa madereva na wamiliki tu. Hata serikal yet inakosea sana bila kukaa na wadau na kutengeneza changes hatutaona punguzo la ajari. Kuna watu wanataman kuwekeza kama greyhound au intercape south africa nan wa kuleta irzar i8 halafu kabla ya kuanza safar inabidi akatwe tako,rejea ilasi express. Kwq wasio jua bus mfano wq irzar ina mfumo wa mpaka kumuepusha dereva na ajali ila ndo £350000. Au intercape south wanamfumo wa gari inapozid 95 alama inalia ofisin na inajikata . nani wa kuweka huo mfumo kwetu wakati kabla hajafika kibaha trafiki ashampiga fine ya kutembea 55 na kibao hakipo
 
Tunahuzinika huku umeanza siasa

una mtoto wewe ngedere wa mjini. wazazi wana shindwa kula, kuvaa, kustarehe ili watoto wasome wewe unaanza kuchokonoa

itabidi upate na wewe ajali ukatike vidole vyote alafu ndo utajua maana ya ajali
Nadhani una matàtizo je ni wewe tu mwenye uchungu una hakika gani kama sijapotelewa na ndugu. Nashukuru mimi ni ngedere wa mjini, je we ni nani,l? Changuduo wa mjini?shoga wa mjini?au choko wa mjini
 
Tunahuzinika huku umeanza siasa

una mtoto wewe ngedere wa mjini. wazazi wana shindwa kula, kuvaa, kustarehe ili watoto wasome wewe unaanza kuchokonoa

itabidi upate na wewe ajali ukatike vidole vyote alafu ndo utajua maana ya ajali
Kuwà mstaarab nimepoteza watu wawili kwa ajali mbili ya jana na juzi halafu unaleta ukungu wako
 
Back
Top Bottom