Vyandarua vyafanywa uzio wa bustani ya mbogamboga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyandarua vyafanywa uzio wa bustani ya mbogamboga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Remmy, Sep 29, 2010.

 1. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Jamani vita dhidi ya malaria, UKIMWI kama watu wenyewe hatutakuwa tayari, haitafanikiwa. Mkazi mmoja wa Kyela atumia vyandarua vya hati punguzo kuwekea uzio wa bustani yake ya mbogamboga. Haya jamani ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni.
   
 2. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #2
  Sep 29, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Hayo ndiyo matatizo ya watu kupewa vitu bure bila ya uchungu wo wote.

  Hivi kweli lazima huyo mkulima atumie vyandarua kuzungushia uzio? Hayo ni matumizi mabaya ya chandarua na ingefaa akaelimishwa kwamba anavyofanya sio vizuri.
   
 3. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #3
  Sep 29, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  mwingine huyu,yaani nishaona wengi wakifanya hivi kuzuia vifaranga visichukuliwe na m[​IMG]wewe.
   
 4. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Haya jamani, haya ndo ya dunia. Nawaomba wahusika wamchukulie hatua kali.
   
 5. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Kweli akili ni nywele kila mtu ana zake. Ubunifu ni muhimu wakati mwingine.
   
 6. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Remmy huu si ubunifu bali ni uharibifu unaotokana na kupewa vitu vya bure. Mtu akipewa vya bure mara nyingi huwa havithamini.

  Nakumbuka moja katika hotuba za Nyerere za zamani alikuwa anaeleza jinsi wakulima walivyokuwa wakipewa mbolea za kukuzia mazao bure/heavily subsidised na Serikali. Kwa vile walikuwa wakiogopa wasionekane kupinga wanachukuwa mfuko wa mbolea na kuutoboa halafu wanauweka kwenye baiskeli. Anatembea na mfuko wake huku mbolea inamwagika kwa hivyo akifika nyumbani hamna kitu. Leo hii watu wamejua thamani basi wanautafuta huo mfuko wa mbolea.

  Case hii ni sawa na hii ya vyandarua ambavyo watu wanafugia kuku.
   
 7. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #7
  Sep 30, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Remmy kweli ni ubunifu, lkn usiofaa!jamani wangekuwa wamenunua kwa pesa zao wasingefanya ubunifu wa namna hiyo.Watu wanapaswa kuelimishwa zaidi na kupewa condition wanapopatiwa net hizo.
   
 8. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #8
  Sep 30, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Nyie naona mnatazama jambo hili kwa upande mmoja tu! neti zinatumika sana, tatizo ni kwamba zimekuwa nyingi mno kuzidi mahitaji.
   
 9. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #9
  Sep 30, 2010
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo demand ikizidi supply inabidi kwenda kinyume chake siyo?sasa Amoeba unataka kuniambia familia moja wameshapewa net nyingi kiasi kwamba hawajui wazifanyie nini zaidi ya kufanya ubunifu huo wa fancy,na kufunika kuku?!kweli bado tuna safari ndefu lkn Mungu ni mwema atafanya kitu.
   
 10. F

  Froida JF-Expert Member

  #10
  Sep 30, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Hawa wanyaki ni malaria sugu kweli na ndiyo hasara ya kupeleka miradi wakati wenyewe hawaoni faida yake ha ha
   
 11. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Ni kweli safari bado ndefu mkuu,
  Wewe nyumbani kwako mko 4, unachoma gunia zima la vitumbua ili kufurahisha watoto!!! Ukikuta watoto wanavipiga kama mipira utafikiria nini..........? thin think think, THINK HARDER! Hizi kampeni zingine hazina maana, wanagawa neti za futi4 mjini, tena neti zenyewe ngumu kama singa-hivi umeshaziona? Umeshafikiri vipi ikiwaka moto!? THINK! Mmbo ya afya hayatakiwi kuingiza siasa, na mimi binafsi siamini kama neti pekee ndy kinga ya malaria, vp mida ya jiioni kabla ya kulala wakati mnaangalia tamthilia? THINK, SI KUFIKIRI MUNGU PEKEE!!!
   
Loading...