Vyama vya upinzani ni taasisi za ulaji? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyama vya upinzani ni taasisi za ulaji?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by thatha, Dec 28, 2011.

 1. t

  thatha JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2011
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Ndani ya CUF kunafuka moshi mweusi unaotishia uhai wa chama hicho...kikubwa kinachosababisha mgogoro huo ni ulafi na uroho wa madaraka. Hamad Rashid anasigana na viongozi wakuu wa chama akiwamo katibu mkuu wake SEIF SHARIFF HAMAD baada ya Hamad Rashid kutangaza kuutaka ukatibu mkuu. Hali kama hiyo inaendelea ndani ya NCCR ambapo David Kafulila na wenzake wamefukuzwa uanachama baada ya kumtaka mwenyekiti wao aachie ngazi kwa kuwa amekidhoofisha na amekosa mvuto.kikubwa hapa ni baada ya Kafulila kuonekana kuutaka uenyekiti wa NCCR.kafulila alinyang'anywa madaraka CHADEMA akaamua kutimkia NCCR.Mwenyekiti wa TLP Augostino Lyatonga Mrema nae hivi karibuni amemtimua katibu mkuu wake JESSE Makundi pamoja na naibu katibu mkuu Hamad Tao.Katika CHADEMA siku za hivi karibuni tumeshuhudia chama hicho kikiwafukuza uanachama madiwani wake watano huko Arusha kitendo kilichowafanya wakose nafasi hizo.yote haya yanatokea huku kila mhusika katika mgogoro akidai ndie ana haki lakini upande unaopingana nae unamuonea.


  My take; Je vyama vya upinzani ni taasisi za kujipatia madaraka ili kujipatia ulaji?
   
 2. k

  kkitabu Senior Member

  #2
  Dec 28, 2011
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 122
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Chadema haiwezi kulinganishwa na vyama vingine including CCM tazama jinsi walivyojitahidi kuwarudisha madiwani kundini lakini wao wakajiona wana haki zaidi kuliko viongozi wetu watukufu wa chadema. Suala la madiwani WA CHADEMA halikushugulikiwa sawa na la Kafulila kule NCCR. Kwa hiyo kama umekula hela za watu ili ulete ujinga wako umu JF uzirudishe.
   
 3. t

  thatha JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  hili la kufukuzwa kwa Hamad Rashid wa CUF linatupa funzo gani katika siasa za bongo.inawezekana ikawa ndio jibu sahihi kwamba alitaka kutupa kitumbua cha mwenzake katika mchanga akawahiwa yeye.ivo maslahi kwanza,mwanachama baadae katika vyama vyetu hapa tanzania.
   
 4. t

  thatha JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  wewe ni vuvuzela tu kaka hata hujui uko wapi na unakwenda wapi.hapa tz kuna NGO'S za Kisiasa hakuna vyama vya siasa.we umekuta NGO ina mkurugenzi unafika hapo unajifanya mjuaji unataka nafasi yake,we unajua malengo yake?tulia kaa chini fanya utafiti,usikurupuke utaumbuka.matusi hayasaidii sana.
   
Loading...