Vyama vya Upinzani na Taasisi za Kiserikali. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vyama vya Upinzani na Taasisi za Kiserikali.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Steve Dii, Sep 16, 2010.

 1. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2010
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Mara kwa mara tunapoongelea kujiimarisha kwa vyama vya upinzani tunakuwa tunaongelea ni namna gani vyama hivyo vimesambaza matawi na mashina yake kwa wananchi, mijini na vijijini. Jambo moja ambalo tunaonekana kutoliongelea au kulisahau ni - namna gani vyama vya upinzani vimejikita katika kuwa na wawakilishi ndani ya asasi na taasisi mbalimbali za serikali.

  Hatuliongelei hili kwani ni kweli umuhimu kwa vyama hivi ni kwanza kuwafikia wananchi, hivyo swala la kujikimu kuwa na wawakilishi kwenye organ mbalimbali za serikali na hata binafsi linakuwa jambo lisilowekewa kipa umbele (tertiary).

  Kujitokeza utata katika matumizi ya ndege ya serikali inayosemekana kukodishwa na Mama Salma Kikwete katika ushiriki wake kwenye kampeni za CCM ili kushawishi wananchi wamchague tena Mh. Kikwete kumenifanya niongelee hili. Jambo lililojitokeza ni utata wa stakabadhi za malipo zilizotolewa kuhalalisha jambo hilo. Stakabadhi hizo zinaonesha utata mwingi hata kwa mwonekano wake tu katika picha.

  Basi, ni jambo hili la utata wa ankara za malipo limenifanya nijiulize kiwango cha uwakilishi wa vyama vya siasa vya upinzani ndani ya taasisi zetu mbalimbali. Tunajua kuna vyama vina wanasheria wazuri sana tu, vile vile kuna vyama vina madaktari wazuri pia. Lakini je, kuna jitihada zozote zile katika kuhakikisha nyanja zote muhimu zinawakilishwa? Mfano, kwenye mabenki, wizara ya elimu, mifugo n.k. Mithili ya uwepo wa baraza kivuli la mawaziri ndani ya Bunge.

  Swala la uvurandaji wa risiti kama linavyoonekana hivi sasa ni sharti lifatiliwe kwenye mtiririko wake wote. Je, vitabu vimechapishwa wapi na lini, je agency amelipa kodi kulingana na mapato aliyoorodhesha? Je, vishina vya risiti na kumbukumbu zake zinafanana au kuonana na kumbukumbu kwenye vitabu vya TRA? Pesa za kigeni na matumizi yake kwenye kampeni zimetokea wapi ndani ya CCM - ni michango kutoka nje ya nchi au wahisani na benki za nje??! Recors za matumizi ya CCM zinaoana na michango inayotolewa kwa chama? n.k.

  Hivyo basi, ni pale vyama vyote vitakapokuwa na wawakilishi wake kwenye taasisi zetu zote, wa kutambulika na wale wasiotambulika, ndipo hapo tutakapokuwa tumekata tawi jingine lililojaa fitna kwenye Taifa letu na kuwa chanzo kikubwa cha matunda yenye kashfa.

  Steve Dii
   
Loading...