Vyama vya siasa vyaruhusiwa kujihesabia kura Kenya

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Tume ya uchaguzi nchini Kenya imekubali kuruhusu vyama vya kisiasa kujihesabia kura kwenye uchaguzi mkuu ambao utafanyika tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.

Hata hivyo tume hiyo ilisema kuwa ndiyo ina ruhusa ya kutangaza matokeo ya mwisho.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga alizua wasi wasi mwishoni mwa wiki baada ya kuwaambia wafuasi wake kuwa muungano wa upinzani wa Nasa, utabuni kituo chake cha kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.

Viongozi wa upinzani wanasema kuwa kuwepo kituo hicho itasaidia kuzuia udanganyifu kwenye uchaguzi.

Rais Uhuru Kenyatta anawania uchaguzi kwenye muhula wa pili na anatarajia kuukabili mungano wa vyama vikuu vya upinzani.

Chanzo: BBC/Swahili
 
IBC WAMEINGIA CHAKA SANA KUWARUHUSU NASA KUJUMLISHA KURA NA KUWA NA KITUO CHAO ITAKUWA NI VIGUMU KUWAZUIA KUTANGAZA KWANI LAZIMA WATAKUWA NA NJIA YA KUYATANGAZA HATA KWA NJIA YA MITANDAO YA KIJAMII..
UAMUZI HUU UTAWAGHARIMU SANA WAKENYA NA IBC WATAUJUTIA KABISA MAANA NASA LAZIMA WATATANGAZA MATOKEA NA HASA WAKIANZA KUONA WANASHINDWA WATAANZA KUYATANGAZA NA HILO LITALETA MKANGANYIKO MKUBWA NA KUZUA VURUGU KABISA.........

IBC KWA MANUFAA YA WAKENYA WABATILISHE KABISA MAAMUZI HAYO MAANA ODINGA HATOKUBALI KUSHINDWA HATA KAMA AKISHINDWA.

IBC WAMEFANYA MAAMUZI AMBAYO WATAJUTIA KABISA...
 
Acha kuweweseka hiyo unayoiongelea ni Tume Huru ya Uchaguzi.
 
Waruhusiwe kukusanya na kujumlisha matokeo yao ila si kutangaza kwa njia yoyote ile hasa mitandao ya kijamii, vingenevyo hilo ni bomu linalosubiri kulipuka. Africa hakuna ustaarabu, unaweza ukadanganya na nyumbu na mainstream media zikachukua habari yako neno sahihi kabisa.
 
Back
Top Bottom