Vyama Burundi vyamuomba Mkapa asizungumze kwenye kikao chao

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,061
Hayo wameyasema Jumatatu hii jijini Arusha wakati wakitoa maoni wakati wa kikao cha siku moja kwa ajili ya kujadili hatma ya amani nchini Burundi. Akizungumza na waandishi wa habari siku hiyo nje ya ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC, mmoja kati ya wajumbe wa mkutano huo, Bigirimana Jacquees alisema hawapingani na msuluhishi wa mgogoro huo ambaye ni Rais Mkapa, bali wanachotaka ni kutokuwa mzungumzaji zaidi katika kikao hicho.

Amesema wao wanataka wazungumze wenyewe kwa wenyewe kwa kutumia lugha zao na kunyoosheana vidole, badala ya msuluhishi huyo kuwa mzungumzaji zaidi.

Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini Burundi wanaoshiriki vikao vya usuluhishi jijini Arusha, wamemuomba msuluhishi wa mgogoro wa kisiasa nchini Burundi, Rais mstaafu Benjamin Mkapa kutokuwa mzungumzaji katika kikao hicho, bali awe msikilizaji zaidi.

“Tunataka amani katika nchi yetu na hatutaki migogoro baina yetu na Warundi wakisikia tumemkataa msuluhishi wetu wanahuzunika sana, lakini tunachomuomba atupe nafasi ya kuzungumza sisi wenyewe kwa wenyewe badala ya yeye kuzungumza sana,” alisema Jacquees.

x11-3.jpg.pagespeed.ic.XO8OY_74bH.jpg


Awali mmoja kati ya mawakili wa kujitegemea kutoka Burundi, Ali Mbongo amesema Warundi wanahitaji amani ikiwemo Kiswahili kupewa kipaumbele kwani pia katika nchi hiyo kuna kabila la waswahili ingawa halipewi nafasi yoyote kwa ngazi za jamii.

Amesema waswahili hao walifika Burundi zamani, lakini cha ajabu hawapewi nafasi yoyote ya uongozi wala kusikilizwa, lakini ni raia wa Burundi na wanapata taabu kutokana na kutotambuliwa kisheria.

Aidha alisema Rais Mkapa aliongoza kikao kilichofanyika mwaka jana Burundi kwa kupeleka maazimio yao kwa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), lakini kuna mambo aliyasema ambayo hawajapendezewa nayo ingawa hakuwa tayari kuyataja, ila alisisitiza ni muhimu wao kama makundi ya vyama vyake vya siasa kusikilizwa wenyewe kwa wenyewe.

Waandishi wa habari hawakuruhusiwa kuingia kwenye mkutano huo wa siku moja, hali iliyosababisha kutojua maazimio ya kikao hicho.
 
Tatizo la msuluhishi anaekuwa ana base upande mmoja....ambae badala kuwa msuluhishi anawashambulia wapinzani wa burundi........badala ya kusikiliza pande zote na kuwasaidia.....kupatana yeye anakuja na maamuzi yake mfukoni!!!
 
BMK asidhani utulivu na amani ambayo ni hulka ya waTz inaweza kuwalaghai na Warundi wasidai haki zao !!!. Kwa maoni yangu Warundi hawahitaji UNAFKI
 
Ha ha sisi huku kwetu tushazoea hata kutukanwa tunaona poa tu ile kwingine wakisema wamesema
 
Tatizo la msuluhishi anaekuwa ana base upande mmoja....ambae badala kuwa msuluhishi anawashambulia wapinzani wa burundi........badala ya kusikiliza pande zote na kuwasaidia.....kupatana yeye anakuja na maamuzi yake mfukoni!!!
yeye hapo upande wa nkuruzinza sio kuleta usawa
 
Inakuaje unakua ma mediator au arbitrator ambaye kabla hata hajawasikilizeni ame pick side?naye anakua sababu ya kutoelewana kwenu kwanza haya mambo ya conflict resolution mkapa kayajulia wapi?
 
Kazi ya mediator ni kufacilitate negotiation tu.Yeye anatakiwa awape nafasi hizo pande kujadili kwa lolote na chochote wakati yeye akisaidia kuwepo na amani wakati wa uzungumzaji wako sasa yeye kageuka kuwa arbitrator?
 
Back
Top Bottom