Inanishangaza kuona hawa wafugaji na mifugo yao wanavyotaka kufanya Tanzania iwe jangwa kwani wanasambaa kama viwavi jeshi sehemu zote zenye rutuba Tanzania..Wafugaji hawa ambao ni wasukuma mazingira ya kwao yaani shinyanga kwa sasa ni jangwa na wanaendelea kuharibu mazingira mengine yaliyosalia kwa madai wao ni watanzania wanauhuru wa kwenda popote Tanzania.Naishangaa serikali inavyolifumbia macho jambo hili hatari nahisi viongozi wanapewa rushwa mifugo hao hao ili waendelee na uharibifu .Nimewaona Morogoro, Mbeya, Iringa,Mtwala,Rukwa,Pwani na kwingine kwingi.Na mara wafikapo maeneo hayo wanaanza kudai haki zao na kuanza ugomvi na wakulima huku serikali ikiwatetea kuwa wanahaki ya KUHARIBU MAZINGIRA.Ndugu watanzani mnapaswa kujua ya kwamba huu uharibifu wa mazingira unatuathiri sisi sote.Na hawa wafugaji hawakumbuki kupanda miti mazingira waliyotoka na pili wanazidi kuongeza idadi ya mifugo.WATANZANIA WOTE TULIONE HILI KUWA NI HATARI KWA TAIFA LETU ,TUTUNZE MAZINGIRA KWA FAIDA YETU NA VIZAZI VIJAVYO.