Vurugu za mabunge duniani

Vurugu za mabunge duniani

Sumasuma

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2011
Posts
342
Reaction score
110
Vurugu si tu za kuzomea bali hata za kupigana na kuharibu vifaa vya ukumbi wa Bunge hutokea katika mabunge kadhaa duniani.
Kwa mfano, Novemba mwaka 2008, vurugu zilizuka katika Bunge la Ukraine wakati baadhi ya wabunge walipotaka kushinikiza kupigwa kura ya kumwondoa Spika wa Bunge hilo, Arseniy Yatsenyuk.
Bunge la Mexico pia liliingia katika rekodi ya vurugu, Desemba mwaka 2006, vurugu hizo zilikuwa zikionyeshwa moja kwa moja (live) na kituo cha televisheni nchini humo huku wabunge wakitwangana ngumi.
Juni, 2010 nchini Nigeria, ngumi zilipigwa baada ya baadhi ya wabunge kusimamishwa ubunge kutokana na shutuma walizopata kuzitoa kwamba Spika wao alikula rushwa.
Bunge la Korea Kusini ndiyo mara kadhaa limepata kuwa uwanja wa mpambano wa ngumi. Machi, mwaka 1998, wakati wa upigaji kura za kumuidhinisha Waziri Mkuu Kim Jong-pil, baadhi ya wabunge walirejesha karatasi tupu za kura zikiwa hazikuandikwa chochote, na hapo ngumi zilianza baada ya baadhi ya wabunge kutaka kura hizo zitambuliwe zimeharibika, na wengine wakibisha.
Zimewahi pia kuzuka vurugu wakati wa jaribio la kutaka kumng’oa madarakani, Machi 2004, Rais wa nchi hiyo, Roh Moo-hyun, wabunge wafuasi wa Rais wakitwangana na wabunge wa upinzani.
Lakini Julai, mwaka 2009, ngumi zilipigwa bungeni Korea Kusini baada ya kutokea mvutano kuhusu Muswada wa Mabadiliko katika sekta ya vyombo vya habari.
Katika mvutano huo, wabunge wa upinzani walitanda na kuzuia njia ya Spika kuingia bungeni, na wabunge waliokuwa wakipinga kitendo hicho waliinuka na kuanza mpambano, lakini hatimaye muswada huo ulipitishwa.
Huko Taiwan, sehemu inayokusudia kujitenga na China ili iwe nchi rasmi inayotambulika duniani, vurugu ziliwahi kutokea katika Bunge lao.
Huko, mwaka 1995 iliwahi kuelezwa kwamba pengine baadhi ya wabunge wangepewa nishani ya Nobel kwa kuwa mstari wa mbele kupambana kwa ngumi bungeni badala ya kuchambua mambo kwa ajili ya kukabiliana na mataifa mengine katika masuala mbalimbali, yakiwamo ya maendeleo.
Machi, 2004, vurugu ziliibuka kati ya wabunge wa upinzani na chama tawala, baada ya kuwapo mvutano wa kutaka kura zilizopigwa wakati wa uchaguzi wa rais zirudiwe.
Lakini Mei, mwaka 2004, wabunge Chu Hsing-yu na Lai Ching-teh, walitwangana ngumi baada ya ubishi kuhusu taratibu za Bunge, huku vituo ya televisheni vikionyesha Mbunge Chu, akimkwida mwenzake, Lai, huku akijaribu kumpiga ngwara.
Katika Bunge la Uingereza imewahi kutokea wabunge wa upinzani na wale wa upande wa utawala kuchorewa mstari wa kuwatenganisha bungeni kwenye zuria.
Mstari huo mwekundu ulichorwa mbele ya mabenchi ya pande hizo mbili, mbunge wa upande mmoja hakuwa akiruhusiwa kuvuka kwenda upande mwingine, ikihofiwa anaweza kuvuka kwenda kumshambulia mbunge wa upande mwingine, na kwa wakati huo wabunge walikuwa wakiruhusiwa kuingia na silaha bungeni.
Vurugu nyingine zimewahi kutokea mwaka 1972 katika Bunge la Uingereza na mwaka 1976.
Marekani, Februari mwaka 1798, kuliwahi kuzuka vurugu, msingi wake ukiwa ni katuni ya kisiasa na hatimaye kuzua ugomvi kati ya wabunge Roger Griswold kutoka Connecticut na Matthew Lyon.
Wakati huo huo, mwandishi wetu Hafidh Kido anaripoti kwamba Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willbrod Slaa amewataka wabunge wa chama hicho kususia kikao cha Tume ya Haki na Madaraka ya Bunge, ikiwa wataitwa kujieleza kutokana na mambo yaliyotokea bungeni jana na juzi, hadi hapo Spika wa Bunge, Anne Makinda atakapotoa hadharani matokeo ya rufaa kumi walizoweka tangu Makinda kushika kiti hicho.
Akizungumzia msimamo wa CHADEMA mbele ya waandishi wa habari katika Makao Makuu ya chama hicho jana, Dk Slaa alitamka kulaani kiti cha Spika na wale wote wanaoendesha majukumu yao katika Bunge la Tanzania kwa kufuata matakwa ya vyama vyao.
“CHADEMA tunalaani kiti cha Spika na wale wote walioonyesha ubaguzi wa wazi katika kuondoa hoja tatu za wabunge John Mnyika (CHADEMA), James Mbatia (NCCR-Mageuzi) na Dk Hamis Kigwangala (CCM) kinyume na kanuzi ya Nane ya Bunge inayotamka Spika hatakiwi kuwa na upande,” alisema Dk Slaa na kuongeza:
“Ninachotaka kuwaeleza wabunge wangu wa CHADEMA, ikiwa wataitwa katika Tume ya Haki na Madaraka ya Bunge wasiende. Wamweleze Anne Makinda wapi zilipo zile rufani 10 zilizokatwa na CHADEMA tangu aingie madarakani. Kwanza watoe majibu ya rufani hizo tulizokata, tena mbele ya ukumbi wa Bunge baada ya hapo wabunge wangu watakuwa tayari kusimamishwa mbele ya tume hiyo.
“Kinachotokea sasa bungeni mjini Dodoma ni kuendesha vikao vya Bunge kwa chuki, uongo na kutofuata haki. Bunge ndiyo sehemu ya kupatikana haki na kutungwa sheria lakini pamegeuka kichaka cha udhalilishaji, uovu, chuki na ubaguzi wa kichama.
“Enzi za uspika wa Samwel Sitta kulikuwa na ubabe kidogo lakini namsifia Sitta kwani hakupenda kupindisha haki na kanuni za bunge ni bora Sitta angeendelea kuwa Spika ni mtu makini sana. Bunge haliwezi kuwa na haki wacha nikuchekeshe kamati ya uongozi wa wabunge wa CCM ina wajumbe 18 ambao ni viongozi wa kamati kuu ya chama chao. Katika kamati hiyo hata maspika wanaingia hoja zote zinazotakiwa kujadiliwa katika kikao cha bunge lazima zijadiliwe na kamati hiyo ya wabunge 18 wa CCM unadhani lini haki itapatikana, lazima tuzichukue hoja zetu na tuzipeleke kwa wananchi na tukifanya
 
Back
Top Bottom