kwa mujibu ya katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania kuandamana ni haki ya kila mwananchi ili mradi afuate taratibu.miongoni mwa taratibu ni kutoa taarifa mapema polisi kwa ajili ya ulinzi na sio kuomba kibali kama wengi wanavyopotosha.
Polisi wametekeleza amri halali kwa mujibu wa Katiba na Sheria, wanasiasa wamekuwa mifano mibaya kwa jamii, namna hii itarudisha usawa na haki.
Haiwezekani wakivunja sheria wanaachwa, sisi uraiani iwe nongwa.
Wapigwe tuu
Wewe unae mwita Mungu mpumbavu huna akili huja soma.Hufai hata kuwepo duniani mwandawazimu kubwa jinga tumbo kubwa umekosa hata elimu
Wajerumani juzi wameadhimisha siku ya mauaji ya kimbari yaliyofanywa na Nazi miaka 70 iliyopita, na maadhimisho hayo yaliisha salama duniani kote. Kwanini hapa kwetu iwe haramu kwa CUF kuwakumbuka wanachama wao waliokufa miaka iliyopita? Mauaji ya Wayahudi hayakuwa halali sawa na mauaji ya wana CUF Zanzibar, lakini inawezekanaje ya Wayahudi kule Ujerumani ambayo ni mabaya zaidi yaweze kukumbukwa bila kusababisha fujo lakini yale ya Zanzibar yazuiwe eti yataamsha hamasa za wananchi?
tbc taifa wamekata.
Kukidhi ufuasi wa CCM lazima 'uchizike' na uwe 'Mpuuzi'!
Sawa lakini turuhusu jeshi la polisi lifanye unyama bila ya sheria kufuatwa??
Hili bunge lina matatizo kuanzia spika hadi wabunge wenyewe.Bunge lina agenda ambazo zilipangwa kujadiliwa.Sasa linatokea tukio mtaani wanaahirisha na kuacha ajenda kuhamia matukio ya barabarani.Waliokamatwa watapelekwa mbele ya vyombo vya sheria kutakakojulikana kama CUF walikosea au la.Bunge kiherehere chake cha nini? wanajadili nini wakati suala liko mikononi mwa vyombo vya sheria?
Bunge limekuwa linaanza kwenda na matukio badala ya ajenda zilizowapeleka pale.Hizi zote ni mbinu chafu za kutaka kuzidisha siku na kula posho zitokanazo na kodi za wananchi.
Hili bunge hovyo kabisa heri uchaguzi uje upesi wachaguliwe wabunge wengine wapya kuliko hawa wa sasa.LO.
Katika maigizo yanayoendelea Bungeni inasikitisha sana Bunge kutojari muhimili mwingine na kujiona wao ni wao na hakuna mwingine.
Hivi inaingia akilini kuanzisha fujo Bungeni kisha eti hoja aliyoleta Mbatia ahijadiliwi leo na kusababisha shughuli za Bunge kusitishwa?. Chukuliwa kila upande uwe na msimamo na tuone utakao shindwa, mimi nimesema hoja itajadiliwa kesho na wewe unasema ijadiliwe leo, wakati huo mimi ndo nimeshikilia rungu itawezekana kweli wewe kushinda bila kutumia busara?.
Kinachosababisha upinzani kupata misukosuko ni kutotii sheria na kujitungia za kwao "Nguvu ya umma" na kusahau kama watakimbilia kule wanakokutukana na kuomba msaada.
Rejea maneno ya kanga anayoyatoa Dr. Slaa akiwa jukwaani juu ya Jeshi la Polisi utafikiri anawashambulia watoto wake na kujiona ananguvu nyingi kuliko wao. Ilifikia wakati anataka kujifanananisha na Nyerere eti mbona nimefika hapa polisi walikuwa wapi?. Vivyo hivyo na Lipumba, ahaiwezekani mkubaliane maandamano yasiwepo kisha ukaandamana kwa kisingizio cha Nguvu ya umma. Kuvunja sheria hakuangali Nguvu ya umma wote kwa pamoja lazima tutii sheria ili tuishi kwa amani.
Sasa Serikali imechoka kuona inazalaurika kila wakati tumeamua kufanya kazi, haiwezekani Bunge kujiona eti wao ndio muhimili Bora kuliko yote kisa eti walishinikiza sakata la Escrow kupitishwa kihovyohovyo na kusababisha hasara kubwa kwa Serikali bila faida yeyote sasa basi na lolote na liwe.
Ushauri kwa Upinzaji kama inawezekana adui lazima uishi nae vizuri ili umshawishi kirahisi akuamini na kukupa madaraka ya kumtawara ama kumuongoza bila kutumia nguvu nyingi. Tumie ujuzi aliotumia Nyerere hadi Wakoloni wakamwamini bila kutumia nguvu, kama mambo yataendelea hivi Watanzania hawatawaamini kwani watahisi harufu ya vita mbeleni, hivyo lazima umimi uwatoke kurudi kwenye sheria na kuteka Jeshi kimawazo.
Na mwisho lazima kutambua kuwa kwenye migogoro hiyo Serikali ina watu wake ili kupunguza ukali wa hoja zilizopo vichwani mwa watu.
Haya ni mawazo yangu tu kama tata mura.
hapo mtuhumiwa ni serikali na serikali ndiyo inastahili kutoa majibu na majibu huenda yakawa hayapo hapohapo wanapotaka yatolewe. hivi kama sio kutaka shari na umaarufu bangi, kesho kuna umbali gani hadi lazima iwe leo na sasa hivi???
halafu mbona makinda katumia busara ya kupita kiasi katika hili..!!!
binafsi naunga mkono kipigo alichopata lipumba maana maandamano yalikuwa batili na sababu ya maandamano ndio ushenzi mtupu.
ningekuwa mimi ndio serikali, katika mwaka wa uchaguzi kama huu ningepiga marufuku maandamano maana kuna WAJINGA KAMA WEWE AMBAO MNAWASHWA NA KUKUNWA KWENU NI KUPIGWA VIRUNGU
Tatizo sio kuvunja sheria,,, tatizo ni kudeal na huyu mkosaji ambaye hana silaha,,, kuna tatizo kwa askari wenu namna ya kudeal na watuhumiwa.. hapa ndio kwenye shida... Mvunja sheria anashughulikiwa vipi??? Ukivunja sheria kwa hiyo upigwe na hamna namna nyingine???