Vua gwanda na gamba vaa uzalendo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vua gwanda na gamba vaa uzalendo!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mkereketwa_Huyu, May 27, 2012.

 1. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,118
  Likes Received: 1,208
  Trophy Points: 280
  Hicho kichwa cha habari hapo juu ni maneno aliyonena kijana Vuvuzela nambari one wa CCM Tanzania nzima (Nnape Nnauye) huko BK. Kwanza najiuliza, huyu vuvuzela ana mawazo gani kwa kuongea haya? Maana kila nikiangalia picha, naona ni CCM ndiyo hawana uzalendo na hili taifa letu. Umasikini, ufisadi, ujinga, ulimbukeni, illiteracy, na ushenzi kibao hapa Tanzania ni wao ndio wameleta. Miaka 50 sasa toka tupate uhuru lakini mpaka leo hii maji ni issue kwenye hili taifa. We umeona wapi mtu akipata maji siku tatu mfululizo anashangaa na kufanya pati wakati ni haki yake, kwani maji ndo uhai wenyewe. Suala la Tanesco ni mchezo ambao naamini kabisa hata Mh. rais anashriki. Nasema hivyo kwa sababu haiwezekani kila anayemchagua aendeshe pale anaiba na kufilisi shirika lakini hakuna anachokifanya zaidi ya kuangamiza Tanesco lakini Mh. rais anakaa kimya kana kwamba anahafiki ule ujinga uliopo pale. Sijasikia kumfunga ama kumyonga kiongozi yeyote mwizi serikalini ili atoe onyo kwa wengine yeye anawachekelea tu na kuwahamishia kwingine ili waibe zaidi. TRA ndiyo kumeoza kabisaaaaa, pale utapeli nje nje na kuna watu wanarundikana tu pale na kazi wanayoifanya haijulikani. Mh. rais anayajuwa haya lakini bado anafumba macho mpaka sasa. Yeye kama rais anashindwa nini kutuma wapelelezi pale? CCM inabidi ipigwe chini tu kwa kutunyonya na utawala mbovu, people learn through mistakes na kweli tulifanya mistakes kubwa sana huko nyuma mpaka tukafika hapa tulipo lakini bado mistakes ile ile inarudiwa tena kwa makusudi tu ili kutukandamiza sie walala hoi then tunaambiwa/ombwa tujivue magwanda for uzalendo wa kuipenda CCM, come on now Nnape....You must have drunken some Kanyanga there in BK, are You for real? Tanzania ndiyo nchi tajiri shinda zote Afrika mashariki lakini sie ndiyo masikini kutokana na ujinga tunaopachikwa na CCM mara oh sie ni wapole hatupendi ugomvi huku wakitufumba macho na kutulia mali zetu hatimaye kujitajirisha wao na familia zao. Mawaziri, wakurugenzi wa almashauri, mameneja, na makatibu wakuu kibao serikalini ni wezi, Mh. rais na serikali yake inajua haya na hafanyi kitu, kisha leo hii Vuvuzela anatumwa kutudanganya eti tuwe wazalendo, for what? Uongozi mbovu wa CCM ndiyo unafanya baadhi ya vigogo serikalini kutofuata maadili ya kazi zao na kufanya yale yanayonufaisha wao na kutesa raia wa kawaida huku serikali ikikaa bila kuchukua hatua zozote, then wakati wa uchaguzi ndiyo wanapita kuhaha kuhamasisha watu kama afanyavyo vuvuzela. Kwa sasa kwa kweli CCM ni maiti tu inayotembea, watanzania uzalendo umetushinda tunataka mapinduzi. Rais anaona kabisa kuwa kiongozi fulani ama meneja fulani anafilisi shirika lakini hatua haichukuliwi, kwa nini? Rais kaunda Takukuru na Takukuru hii hii ndiyo inayoongoza kwa rushwa hapa Tanzania. Je, Mh. rais amechukuwa hatua gani mpaka hivi sasa? Vuvuzela anataka watu wajivue magwanda na magamba wavae uzalendo, kwa sifa zipi za CCM itazofanya watu tuwe wazalendo wakati ni wao ndiyo wanatupa umasikini? Afrika na dunia nzima watu wamechoka na ndiyo maana kila kukicha kuna vita ama mapinduzi sehemu fulani duniani. Hivi kweli kuna Mtanzania mwenye akili timamu anayetaka uzalendo wa kutawaliwa na CCM leo hii? Kwa kweli CCM ina kazi ngumu kushawishi watanzania kuwapa kura kunako 2015, kweli kazi ipo.
   
 2. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  nape ni kama TOM wa katuni ya Tom&jerry
   
 3. aye

  aye JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,989
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 160
  gamba limemshinda uzalendo atauweza
   
 4. kivyako

  kivyako JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 8,843
  Likes Received: 4,210
  Trophy Points: 280
  Wazee wa kudesa, walikuwa wapi siku zote?
   
 5. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #5
  Aug 10, 2013
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
Loading...