VPL - SIMBA VS YANGA

VPL - SIMBA VS YANGA

Jua usiyoyajua

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Posts
1,166
Reaction score
684
Asiye na mwana aeleke jiwe ndivyo ninavyoanza kusema kuhusu mechi ya leo kati ya watani wa jadi. Timu zote mbili zisibweteke kwani zina nafasi sawa yeyote anaweza kuwa mshindi. Likini yule atakaetumia karata zake vyema kwa maana idara zake zote tokea golikipa, walinzi, viungo, wafungaji hadi washabiki ndiye atalamba dume.

Mpira ni ufundi ndiyo sababu unakuwa na kocha na wala si uchawi na ndiyo sababu kwenye timu hashilikishwi mchawi wa timu.

Umakini uwanjani leo kwa kila timu unahitajika kwa timu zote ili Simba itimize ndoto zake za muda mrefu za ubingwa ilioupoteza kwa miaka kadhaa na Yanga iithibitie dunia wao si mchezo bali ni tishio kwamba kutangulia si kufika kama ambavyo wameiithibitia Simba kwa miaka kadhaa kwenye VPL. Haya sasa kazi kwenu ingawaje ushindi wa Simba ni muhimu zaidi ili mpate lau hizo 80,000,000 za mshindi kwani Yanga wao tayari wanazo mkononi kiasi cha kinachokaribia Bilioni moja walizozipata kwa mechi mbili za kimataifa walizocheza.

Mungu ibariki Simba, mungu inariki Yanga.
 
Kwenye ulimwengu wa roho yanga italala kwa matokeo ya 2-1....
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Matokeo toka kwa babu;0-4. Sijui nani mwenyeji/mgeni kwenye hii game,wote watoto wa kariakoo
 
Hahaaaa. Kila mwamba ngoma lazima avutie kwake. Simba jiandaeni leo lazima pachimbike.

Ila hala hala na viti tu sababu hamchelewi kuja na matokeo yenu vichwani.
 
Back
Top Bottom