Kiufundi: Azam wametawala katikati kwa sababu wamechezesha wachezaji wanne ambao kwa asili ni viungo wakabaji ambao ni Kipre Balou, Mudahir Yahya, Frank Domayo pamoja na Himid Mao tofauti na Simba ambao wapo vijana wawili tu ambao ni Jonas Mkude pamoja na Said Ndemla. Endapo kocha atafanya mabadiliko ya kumtoa winga mmoja na kuingiza kiungo mmoja au mshambuliaji mmoja na kuingia kiungo mambo yatakuwa tofauti na kuna uwezekano wa Simba kutawala na hatimaye kuongeza magoli zaidi.
Timu ya Azam kutokana na kutawala katikati washambuliaji wake wakiwa makini huenda kipindi cha pili wakasawazisha na pengine kupata magoli zaidi.
Kiushabiki: nataka Simba wapate goli la pili na hatimaye kupata ushindi katika mechi hii ya leo.