Hongera kwa uchambuzi, hebu weka na za Yanga....
TFF ni lazima iwe makini zaidi, kwa sasa ligi imegeuka vita. Ladha ya soka safi inapotea na kinachoanza kuota mizizi ni kukamiana na rafu chafu zenye kuhatarisha uhai kwa wachezaji. Itafika wakati tutashindwa kuona tactical holding, piercing and physical confrontation kwa sababu wachezaji wataogopa kukaa na mpira au kulazimisha move kati kati ya msitu wa mabeki kwa kuogopa kilichompata Emanuel Okwi na Amis Tambwe. Kuna njia rafiki za kuchukua mpira kwa adui kama tackling and tactical obstruction ( refa akipeta poa) lakini huu uhuni mtauana. Marefa muwe makini . Faulo walizofanyiwa Tambwe na Okwi technically and tactically zina muathiri mchezaji kisaikolojia.".. tushukuru Mungu Okwi yupo hai hadi sasa, maana alipigwa kiwiko mshipa wa fahamu ulio nyuma chini ya kichwa chake na ndo maana alipoteza fahamu kwa zaidi ya dk 10"
Source: Dr. wa Simba Sc.
Nami pia nategemea kuona hatua kali saaana zikichukuliwa.
Ingekuwa ni mchezaji wa Yanga TFF ingechukua hatua kali za kisheria, lakini kwa Simba waliombea hata afe kabisa.TFF ichukue hatua...OKWI alichezewa faulu mbaya sana ambayo ingeweza kupelekea kifo chake
Sasa tuone TFF na double standards zake
Ikichukua hatua nitashangaa sana....Mkuu kwa Yanga ile ni siasa tu imefanyika....wale jamaa Tambwe na Michae wote walikua wanapeana vikumbo kwa zamu.
Wote wamepigana ngumi za kisiri siri.
Sema tu kwa sababu Yanga ni timu ya Magazeti ndio maana imekuwa vile.
Sasa nataka ushuhudie jinsi TFF ilivyo na Double standard.Katika hili la OKWI kupigwa hadi kuzimia/kukaribia kufa....na hakuwa na mpira.
Nakuhakikishia TFF haitachukua hatua zozote
TFF ni lazima iwe makini zaidi, kwa sasa ligi imegeuka vita. Ladha ya soka safi inapotea na kinachoanza kuota mizizi ni kukamiana na rafu chafu zenye kuhatarisha uhai kwa wachezaji. Itafika wakati tutashindwa kuona tactical holding, piercing and physical confrontation kwa sababu wachezaji wataogopa kukaa na mpira au kulazimisha move kati kati ya msitu wa mabeki kwa kuogopa kilichompata Emanuel Okwi na Amis Tambwe. Kuna njia rafiki za kuchukua mpira kwa adui kama tackling and tactical obstruction ( refa akipeta poa) lakini huu uhuni mtauana. Marefa muwe makini . Faulo walizofanyiwa Tambwe na Okwi technically and tactically zina muathiri mchezaji kisaikolojia.
FAIR PLAY PLEASE
Refa alishindwa kumudu mchezo kwa 99%...Duh kuna viatu vinatembea hapa
Ingekuwa ni mchezaji wa Yanga TFF ingechukua hatua kali za kisheria, lakini kwa Simba waliombea hata afe kabisa.
Kwa marefa hawa TFF na FRAT yake ijiandae kuchukua maiti ya refa siku moja. Mimi ninaamini hawa marefa sio kwamba wanahongwa ila hawana uwezo wa kuchezesha mpira wa miguu.Niliogopa sana pale wachezaji walivokua wanarushiana daruga live mbele ya refaree....zaidi ya mara 5...refa anaangalia tu.
Niliogopa sana Kavumbagu anamsukuma beki kwenye 18 na anampiga teke kipa wakati ameshashika mpira.
Niliogopa sana kuona refa anapotezea tu.
Nikajiuliza huyu refa haoni au kuna nini?
Anataka watu wajichukulie sheria mkononi?
Kwa rafu aliyochezewa Okwi...kupigwa kiwiko akiwa hana mpira...ikiachwa hivi hivi...simba tutajua cha kufanya
Juzi mlikuwa mnashangilia Tambwe alivyopigwa leo kapigwa mchezaji wenu ndio mnagundua kuna shida, wachezaji wa bongo hawajui fair play
Kwa marefa hawa TFF na FRAT yake ijiandae kuchukua maiti ya refa siku moja. Mimi ninaamini hawa marefa sio kwamba wanahongwa ila hawana uwezo wa kuchezesha mpira wa miguu.
Mkuu unakumbuka pale mchezaji wa Simba alipochezewa rafu na kuanguka chini refa alipeta kwa kuwa Simba ilikuwa inashambuliwa, mpira ulipochukuliwa na Simba kuelekea lango la Azam ndipo alipiga filimbi ya kusimamisha mchezo jamaa atibiwe. Hata mtangazaji wa TBC Taifa alimshangaa refa kwa tukio lile.
Mkuu penye ukweli lazima usemwe. Refa aliyechezesha mechi ya Yanga na Polisi alishindwa kuthibiti nidhamu uwanjani matokeo yake mpira ukageuka vita badala ya burudani.
Jana mechi ya Simba vs Azam tuliokuwepo kiwanjani na hata walioshuhudia kupitia Luninga waliona refa kipindi cha pili mpira ulivyomshinda.
1. Lile tukio la Kavumbagu kumpiga teke la makusudi kipa wa Simba Manyika alitakiwa kutoa onyo. Matokeo yake rafu za kijinga zikaanza .
2. Tukio la mchezaji wa Simba kuchezewa rafu na kugaagaa chini lakini refa alipeta kwa kuwa Simba ilikuwa inashambuliwa. Baada ya Simba kunyan'ganya mpira na kuanza kuelekea langoni mwa Azam Refa akapiga filimbi ya kusimamisha mchezo ili mchezaji atibiwe. Inashangaza sana.
3. Tukio la wachezaji kurushiana madaluga upande wa mashariki ya uwanja kama mara nne hivi lilitokea tena mbele ya Refa, mpaka mchezaji wa Simba alipokita njumu kwenye ugoko wa mchezaji wa Azam ndipo refa alipopuliza filimbi.
Kwa matukio hayaTFF kupitia FRAT ina kazi kubwa sana ya kufanya.
Mkuu hakuna mtu aliyeshangilia hapa, kilichofanyika ilikuwa ni kulinganisha alichofanya Tambwe na beki wa Ruvu Shooting na malalamiko yaliyotolewa na Yanga.Juzi mlikuwa mnashangilia Tambwe alivyopigwa leo kapigwa mchezaji wenu ndio mnagundua kuna shida, wachezaji wa bongo hawajui fair play
Ni kweli kabisa mkuu.Nadhani kuna tatizo la msingi la ma refaereee
Nafikiri sio ishu ya kuhongwa
Ni ishu ya Competence na kukosa kujiamini
Kukosa kujiamini (Confidence) katika maamuzi ni tatizo la watanzania wengi
cc Makoye Matale
Yakheeeeeee...kumbe hata kwenye soka upo?goooo azam 7 simba bado hawajapata kitu hapa.aah kumbe naota bado moja moj
Malipo yako duniani hapa hapa. Hivi majuzi mliinyoshea vidole Yanga kwa kulalamikia umafia aliotendewa Amisi Tambwe, mkadai Yanga ni timu ya kulalamikalamika tu. Hata wiki haijapita mmekutana na kigongo cha wiki na kuanza kulalama. Pole sana.
Anyway, tuache utani wala ushabiki, hatua lazima zichukuliwe vinginevyo makubwa zaidi yanaweza kutokea uwanjani.
Mkuu fuatilia post yangu kuhusu rafu alizofanyiwa Tambwe, si kila mwanasimba alifurahishwa na zile rafu, wengine ni waumini wa fair play bila kujali nani hajafanya fair. Hata jana kama ulifuatilia vizuri baada ya rafu aliyofanyiwa Okwi post humu jukwaani zilipungua. Mchezaji anapigwa kiwiko hana mpira mpaka anapoteza fahamu na hakuna kadi iliyotoka na bado kuna wapuuzi wachache wanashangilia na kusema Simba wanatafuta sare kwa hiyo sijui walitaka wachezaji wetu wote wazimie ndo wafurahi, nadhani kuna haja ya wachezaji kufundishwa hata elementary ya mwili wa binadamu na sehemu gani zina madhara unapomgonga mchezaji na wakatazwe kabisa na ikitokea tu mchezaji kafanya hivyo afungiwe mechi kadhaa na faini juu mbona mabondia wamewekewe sheria kabisa hakuna kupiga below the belt kwa sababu wanajua mtu unaweza pigwa viungo vya uzazi, hakuna kupiga nyuma ya kichwa kwa sababu huko kuna mishipa ya fahamu na unaweza kusababisha mtikisiko wa ubongo pia. Haya madhara ya kujifanya kutojua madhara yake unakuta mchezaji mwingine anamgonga mwenzake kwenye uti wa mgongo. Kuna ulazima wa wachezaji kukumbushwa mara kwa mara kwamba mpira sio vita hata vita yenyewe kuna baadhi ya silaha haziruhusiwi.Malipo yako duniani hapa hapa. Hivi majuzi mliinyoshea vidole Yanga kwa kulalamikia umafia aliotendewa Amisi Tambwe, mkadai Yanga ni timu ya kulalamikalamika tu. Hata wiki haijapita mmekutana na kigongo cha wiki na kuanza kulalama. Pole sana.
Anyway, tuache utani wala ushabiki, hatua lazima zichukuliwe vinginevyo makubwa zaidi yanaweza kutokea uwanjani.
Hahahaah,,,,,mkuu una undugu na marehemu shehe yahya????
Nadhani kuna tatizo la msingi la ma refaereee
Nafikiri sio ishu ya kuhongwa
Ni ishu ya Competence na kukosa kujiamini
Kukosa kujiamini (Confidence) katika maamuzi ni tatizo la watanzania wengi
cc Makoye Matale
Huyu bwana anashindwa kujua kuwa Timu ya kwanza na simba zinatofautiana kwa point za gemu tatu tu
Na azam iko mbele kwa gemu moja
Hii simba itawaua kina Makoye Matale mwaka huu