iparamasa
JF-Expert Member
- Nov 14, 2013
- 13,437
- 14,924
Gazeti la THE CITIZEN limeripoti kwamba kampuni kubwa ya simu,Vodacom Tanzania,ina mpango wa kuomba soko la hisa liiongezee muda wa kuuza hisa baada ya kushindwa kufikia lengo.
Tarehe ya mwisho kuuza hisa ni tarehe 19/4/2017
Baadhi ya mawakala kama Orbit Securities walipanga kuuza hisa zenye thamani ya bilioni 200,lakini mpaka sasa wameuza hisa zenye thamani ya bilioni 100.
Vyanzo vinasema Vodacom wanapanga kuomba serikali iruhusu taasisi na watu kutoka nje ya nchi pia wanunue hisa katika kampuni hiyo
(Natambua pia kuna jamaa mmoja japo simkumbuki jina,ameishitaki Vodacom na kuzuia isiuze hisa akidai kwamba na yeye ni mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Vodacom, Vodacom wanamkataa kwamba sio mmiliki,matokeo ya kesi hayajajulikana mpaka itakapoamuliwa na mahakama,sasa sijui mahakama ikiwapiga chini Vodacom,itakuwa na madhara gani kwa walionunua hisa)
Wana uchumi,tunaomba mtupe tafsiri ya mambo hayo,yanaashiria nini? Ila binafsi nilikuwa nataka serikali ifanye moja au mawili
MOJA: Vyama vya ushirika nchini vinayumba sana kimapato hasa pale msimu wa mazao unapokuwa haueleweki,serikali iwaite viongozi wa vyama hivi kama Nyanza,Kilimanjaro Cooperative Union,Kagera Cooperative Union na vingine,iwalazimishe wawekeze Vodacom walau bilioni mbili kwa kila ushirika,au zaidi,hii itafanya diversification ya uwekezaji na kuvifanya vipate mapato ya uhakika kwa miaka mingi ijayo na kuvifanya vihimili mitikisiko ya kiuchumi.
MBILI: Mashirika ya hifadhi ya jamii yawekeze Vodacom,Tigo,Airtel pesa zao baada ya kujiridhisha kwamba zitazaa na watapata faida kubwa kuliko kuziacha fedha hizo zikae tu Benki Kuu ambako zitawatoa mate wakubwa na kuzitumia katika miradi isiyoeleweka
TATU:Ufanyike ubunifu zaidi wa kuwashirikisha wananchi na wafanyakazi wawekeze katika makampuni haya,wafanyakazi wana mishahara, serikali kupitia wizara ya fedha inaweza kuweka dhamana ya,kwa mfano,kuwakata wafanyakazi wanaotaka,katika mshahara,Tsh laki mbili,mpaka milioni kwa kipindi cha mwaka au miezi sita,na mapato hayo yakaenda moja kwa moja Vodacom au kampuni yeyote kama hisa,hii wakifafanuliwa wataelewa na wengi watakubali,hii inaweza kufanywa na serikali na au kwa kushirikiana na makampuni binafsi,watatembelea maeneo wanayofanya kazi na kufafanua na kuwaunga wahusika.
TATU: kila halmashauri ina vikundi vya akina mama na vijana ilivyovisajili,hivyo basi kila halmashauri iwekewe lengo la kuhakikisha vikundi visivyopungua kumi mpaka ishirini wameviita ofisini kwao na kuvishawishi kununua hisa hizo,hii itasaidia serikali iache kuombwa hela na vikundi hivyo au watu hao.
NNE: Makampuni hayo yanayouza hisa yawekewe lengo ya kuwafikia akina mama na vijana kwa asilimia Fulani kama sharti mojawapo,hii itawasaidia kufikia kundi hili ambalo kila Siku limekuwa likipigiwa kelele
TANO: Badala ya kuwauzia watu wa nje hisa hizo baada ya watanzania kushindwa kuzinunua,serikali yenyewe izinunue ili iweze kupata faida,na pia kuchunguza mwenendo wa faida wa kampuni hizo,pia mashirika ya umma wanaweza kununua,itakuwa aibu kwa hisa hizo kuuzwa nje ya nchi kwa sababu sisi tumeshindwa kuzinunua