Baba rai
JF-Expert Member
- Jun 14, 2016
- 228
- 292
Nimekuja Tanga kikazi juzi na pesa yote ya mahitaji na akiba kwa ujumla nimeweka katika M pesa, kufikia usiku kama saa nane mtandao ukakata na kuandika Emergency na hali ikaendelea hivyo hadi jana mchana hali iliyonipa wasi wasi na kutembelea vituo kadhaa vya Vodacom na jibu nililopewa ni kuwa hilo ni tatizo la kimtandao hapa Tanga na litarekebishwa.
Nimetembelea vituo kadhaa vya M pesa na kukuta makundi ya watu wakilalamika na wengine kutoa machozi kulingana na mahitaji ya pesa zao katika mtandao.
Nimelala hatimae imefika leo hali ni ile ile! Vodacom chonde chonde mnaniadhiri ugenini natakiwa kulipa hoteli, usafiri, chakula na mahitaji mengine, kwa nini mnitese na pesa zangu mwenyewe? Tatizo gani lisilo isha tangu juzi? Hii mitandao ya simu si salama kabisa kwa pesa zetu.