Hii inatokana na mtandao unavyofanya kazi, wateja wote wa voda tunashare kiasi kidogo cha extrernal IP addresses, kwa kifupi ISPs wanatumia NAT kukabiliana na uhaba wa IP addresses na kuleta security/anonyimity fulani kwa watumiaji.
Sasa tatizo linakuwa ni kwamba kuna PC moja kwenye mtandao wa Voda iko infected na virus za kutuma SPAM kunakuwa hakuna njia kwa mpokea SPAM kutofautisha ni PC ipi inatuma, kwa vile wanaona external IP tu, ambayo wote tunaitumia, hivyo wakii blacklist hiyo IP wote tunaumia.
Kwenye situation hii ni kwamba kuna PC za Bongo zinatuma SPAM kwa vile ziko infected na Botnet, hivyo IP imekuwa blacklisted
This IP is infected (or NATting for a computer that is infected) with the kelihos spambot. In other words, it's participating in a botnet.
Na hizo forum zinaitumia hiyo blacklist kimakosa, haitakiwi kutumika kublock website access, inatakiwa itumike kudetect SPAM tu.
Suluhisho rahisi kwako ni kuregister account kwa kutumia mtandao mwingine, kama wanablock kwenye registration tu, kisha uwe unalogin kama kawaida kwenye PC yako, pia uanweza kutumia proxy wakati wa kuregister kubadili external IP yako.
Suluhisho la kudumu linabidi lifanywe na Voda kwa kublock Port ya email (25) hii itazuia majority ya SPAM kutoka kwenye network yao.
NATs