Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Uhondo wa patashika ya ligi kuu Tanzania, Vodacom Primier League VPL, umeendelea tena leo Desemba 2, 2019 kwa viwanja viwili kutimua vumbi, ambapo Biashara United wakiwa kwenye uwanja wa Karume mjini Musoma, wamechomoza na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ndanda FC.
Patashika nyingine ilikuwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kwa Yanga SC kubanwa mbavu kwa kulazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya KMC FC
KMC FC ikicheza kandanda safi la kuvutia hasa kipindi cha pili na kuipa presha kubwa Yanga ambao walikuwa wakiongoza kwa 1-0, walisawazisha kupitia kwa Abdul Hillary kwa mkwaju wa penati kutokana na beki Kelvin Yondani kumuangusha Hassan Kabunda kwenye eneo la hatari.
Kwa sare hiyo KMC kwa upande wao ni kama ushindi baada ya kupoteza michezo mitatu mfululizo iliyopita huku kocha wa msaidizi Ahmady Ally akisema ameridhika na kiwango cha timu yake.
Kwa upande wake Kocha Charles Mkwasa amesema wachezaji wake hawakuwa kwenye kiwango kutokana na kuchoshwa na ratiba huku akilalamikia penati ambayo walipata KMC FC.