Vodacom Premier League 'VPL' Simba SC dhidi ya Polisi Tanzania, Rekodi Ya Alama 50 Kuwekwa Leo

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom Premier League VPL, kuendelea tena leo February 4, 2020 ambapo, Simba SC, Wekundu wa Msimbazi, wanawakaribisha Maafande wa Polisi Tanzania, mchezo utakaopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.

Mchezo wa leo ni wa kufunga mzunguko wa kwanza kwa timu zote mbili, unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90.

Simba SC katika mechi 4 zilizopita ameshinda zote huku Polisi Tanzania wakishinda mechi 3 na sare moja hivyo Simba SC, ambao ndo Vinara wa VPL wakiwa na alama 47 wanaingia dimbani wakiwa na lengo la kuvuna alama tatu muhimu ili Kuweka Rekodi Ya Kufikisha Alama 50, kwa mzunguko huu wa kwanza wenye timu 20.

Kocha Msaidizi Suleiman Matola amsema ligi ni ngumu na hakuna mechi ndogo hivyo wamejiandaa kupambana kama walivyopambana katika mechi zilizopita wakiwa na lengo la kushinda ili kujiimarisha pale juu kwenye msimamo.

Naye Kocha Msaidizi wa Polisi Tanzania Ally Mtui, anasema mchezo utakuwa mgumu hasa ukizingatia wapinzani wao kutopoteza mechi nyingi hivyo wanaangalia namna ya kufanya ili kuweza kushinda mchezo huo.

Kumbuka mechi ni kuanzia saa 1:00 usiku, Usikose Ukaambiwa..!

...Line Up Angalia Kwenye Post #20.
IMG_20200204_142603_511.jpeg
IMG_20200204_142620_054.jpeg
 
Taarifa ya hivi punde;

Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC), ya Shiza Kichuya tayari imefika.

Sasa Simba SC ipo huru kumtumia kwa mchezo wowote iwapo kama Kocha atamuhitaji.
 
Vikosi vya leo Simba SC na Polisi Tanzania...Beno akiendelea kuaminiwa kwenye milingoti mitatu..!
IMG_20200204_173852_663.jpeg
IMG_20200204_173912_976.jpeg
 
Back
Top Bottom