Hizi ndiyo sababu kuu maalumu zinazowafanya mashabiki wa Simba SC kugomea kununua tiketi za mchezo wa Simba SC dhidi ya Asec

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,206
12,747
Ukweli usemwe japokuwa ni mchungu, hamasa imekua kubwa sana katika kuwahamsisha mashabiki wa Simba sc lakini mwitikio sifuri.

Zimesambazwa tickets za bure kwenye matawi, viongozi wa Simba sc wanadai kuwa wameshusha kiingilio mpaka elfu 3000 kwa mzunguko Lakini nyuma ya pazia ni bure.

NALIA NGWENA nawapa sababu za mashabiki wa Simba sc kususia kununua tickets za mchezo wa Asec mimos utakaopigwa tare 25/11.

Mosi, kipigo kitakatifu (mbwa mwizi) walichokishuhudia mashabiki wa Simba sc dhidi ya mtani wao, hii imewanyong'onyesha sana mashabiki na kujiona kuwa hawana timu.

Pili, Matokeo mabovu ya Simba sc kwenye mechi za kimataifa, mashabiki wanajua kuwa hata wakihudhuria matokeo mazuri kwao ni sale tu tofauti na hapo labda wachezee kichapo.

Ikumbukwe toka Simba sc ianze kushiriki michuano hii ya kimataifa msimu huu haijawahi kushinda Bali imetoka sale michezo yote mpaka kufuzu makundi.

Tatu, mashabiki hawana Imani na kocha Cadena na msaidizi Wake Suleimani matola, mashabiki wanaamini makocha Hawa walioachiwa timu kwa muda mfupi hawana mbinu za kumfunga Asec.

Nne, uongo wa viongozi wa Simba sc akiwemo msemaji wao Ahmedy ally, kiufupi mashabiki wamechoka na wamemzoea kwa porojo zake zisizo na mashiko ukija kwenye uhalisia hakuna kitu.

Tano, kikosi kibovu Cha Simba sc hili lipo wazi haina kikosi Cha kuwafurahisha Wana Simba sc Bali Wana kikosi Cha kuwapa presha mashabiki wa Simba hii NI moja ya sababu kuu inayoifanya mashabiki wasiende uwanjani.

Maoni Yangu: yakifanyiwa kazi hayo, mashabiki watakuja uwanjani pasipo kufanyiwa hamasa ya visipika.

Nawasilisha hoja.
 
Natarajia wenye Simba yao waseme wewe ni Yanga uliyevaa jezi ya Simba.
 
Mmpewa tuzo ya mashabiki bora, leo hamtaki kuingia. Tajiri kasema kesho ukiwa na MoXtra,Mo Sabuni unaingia mzunguko na atakaye kuja na mche wa sabuni,anaenda kukaa VIP.

Vp na hii offer ya Tajiri hamuitaki.....? maanake unaangalia mpira huku unapata kinywaji, baada ya hapo unarudi gheto unatumia sabuni kuogea.
 
Nawasilisha hoja.
MO apunguza kiingilio Sasa akiona mmegoma kabisa ananunua tiketi zote muende mkaone mnavyofungwa na Assek Mimosa

Kutoka buku 5 mpaka buku 3

Andaa Buku 3 kanunue tiketi Ila mimi kwa nnachokiona nakwambiaje minya hivyo hivyo tajiri atanunua tiketi zote mtaingia bure km alivyofanya yule tajiri wa Congo Moize Katumbi na Tp Mazembe watu walinunuliwa tiketi zote na tajiri wakapewa na bonus juu na Tp Mazembe ilishinda siku ile 😆 Sasa wewe katoe buku 3 mkashuhudie mnavyofungwa
Kalpana
 
MO apunguza kiingilio Sasa akiona mmegoma kabisa ananunua tiketi zote muende mkaone mnavyofungwa na Assek Mimosa

Kutoka buku 5 mpaka buku 3

Andaa Buku 3 kanunue tiketi Ila mimi kwa nnachokiona nakwambiaje minya hivyo hivyo tajiri atanunua tiketi zote mtaingia bure km alivyofanya yule tajiri wa Congo Moize Katumbi na Tp Mazembe watu walinunuliwa tiketi zote na tajiri wakapewa na bonus juu na Tp Mazembe ilishinda siku ile Sasa wewe katoe buku 3 mkashuhudie mnavyofungwa
Kalpana
NGOJA WAJE MAKOLO
 
Break in News:

Platinum tiketi SOLD Out
Wamegawa bure hizi
1700834567821.jpg

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom