Vodacom. Nani kawalogoa

Vodacom. Nani kawalogoa

rushanju

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Posts
3,327
Reaction score
5,594
Ni tangu asubuhi kila nikitaka kuongeza salio simu haitaki. nataka kupiga simu za muhimu lakini huduma yao ya kuchukua hela yangu haikubali kabisaa. Nauliza wana JF hivi na nyie mnapata tatizo kama hilo au ni kwangu tu.
 
voda hawana jipya nahisi wamelewa sifa badala ya kuwahudumia wateja wao na kuwapa taarifa kutokana na matatizo ya mtandao,hujifanya kama hawajui vile kinachoendelea ktk kampuni yao.
 
Ni tangu asubuhi kila nikitaka kuongeza salio simu haitaki. nataka kupiga simu za muhimu lakini huduma yao ya kuchukua hela yangu haikubali kabisaa. Nauliza wana JF hivi na nyie mnapata tatizo kama hilo au ni kwangu tu.
mimi nina wiki sasa.sio voda tu ata tigo wanatatizo ilo
 
Mie wameiba ela yangu ya SIM ya modem wakati ilikua tayari kwene package ya unlimited. Pia watu wengi asubuhi wamekua wakilalamika wakishindwa kutop-up au kupata huduma zingine za kawaida. Nafikiri kwa sababu TCRA wamelala na hawajui wajibu wao, ni wakati wateja tukaanza kuwa-sue watoaji huduma wote wanaotoa huduma fyongo/
 
Sijajua kama ni maeneo nilipo tu au hata kwingine,niko Dodoma lakini tangu nimefika hapa wiki ya tatu voda ukipigiwa unaongea dakika moja au mbili baada ya hapo unaanza kusikia sauti za chupa zikivunjwa mpaka nimeamua kuhama mtandao.
 
Kuna style nyingine unampigia mtu, simu yako inaonyesha amepokea na dakika zinaenda ila mpokeaji humsikii. Na hata ukiwasiliana nae baadae atakwambia hajaona miised call yako wala hajapokea simu yako, imetokea kwa watu kadhaa zaidi ya mara moja.

Mbona huduma ikiwa mbovu vigezo na masharti havizingatiwi?
 
he vyupa tena?
 
kweli kabisa ndugu,mwishoe unaambiwa salio lako halitoshi wakati uliyempigia hajui chochote lakini sms zao za promotion wanatuma masaa yote na zinakufikia,wanaokutafuta sms au calls zao hazifiki,sms unaipata ina siku tatu hewani!
 
Umenunua muda wa maongezi wa Tsh8500 wa kupiga Voda-Voda, kutuma SMS na intaneti kwa siku 2. Kununua tena tuma 1 kwenda 15030. Kujua salio piga *102*27#
NI SMS KUTOKA VODACOM NI YA TAREHE 5/mar2013 mpaka Sasa wamenikata ela yangu lakini sijaipata mpaka Sasa na kila nikipiga sm voda wanasema inashuumhulikiwa mpaka leo sijui nifanye nn
 
Ni kweli. Mm binafsi nme xperience hiyo kitu jana wakati kumpunguzia Mtu Credit kwenye M-Pesa. Voda Mjirekebishe.
 
Wapuuzi sana hawa vodacom, juzi nimenunua umeme kwa M-pesa saa mbili usiku, umeme wamenitumia saa kumi na moja asubuhi, yaani wanakera hadi basi
 
he vyupa tena?

Unashangaa ndugu yangu? kuna siku nilikua naongea na mtu yupo ofisini lakini nashangaa unasikia masauti mithili ya CD yenye mikwaruzo, mahoni ya magari yaani full noice. TCRA na ile sijui tume ya ushindani inabidi waingilie kati.

Nikawa nafuatilia mambo ya kisheria kwenye mtandao wa vodacom, wanakwambia mambo yote ya kisheria yatafuata sheria za UK, unajua inakera sana.
 
Vodacom kuna Tatizo........!
1. Kuhamisha pesa kutoka Mpesa kwenda benki huduma hii haiwezekani wiki ya pili ya sasa WAKO kimya.....!
2. Huduma ya Mpesa is on and off unaweza nunua salio hata mara 4 ndio unapata salio WAKO KIMYA.......!
3. Huduma kwa wateja is WORST I have ever experienced they keep with long stories ambazo hata hatutaki kusia so and so bonyeza 1....it goes 8 unataka kuongea na mhudumu utasubiri for half an hr na humpati mtu wa kuongea nao
4. uko kwenye maongezi simu inakata ghafla eti mtandao umekata ghafla
SHIDA ya nini kwenye dunia ya ushindani na uhuru wa kuchagua
Mimi nimehamia tayari ............... Mtandao gani hawataki kuongea na wateja wao! Eti unaongea na menu tu......
 
Ni tangu asubuhi kila nikitaka kuongeza salio simu haitaki. nataka kupiga simu za muhimu lakini huduma yao ya kuchukua hela yangu haikubali kabisaa. Nauliza wana JF hivi na nyie mnapata tatizo kama hilo au ni kwangu tu.
Aah kumbe nyie siku moja si week ni jambo la kawaida internet ndo usiseme mwezi unaweza kupita hata ukiwapo speed mh(sijui edge bila shaka)
 
Back
Top Bottom