Wick
JF-Expert Member
- Dec 19, 2012
- 8,313
- 12,166
Juzi nimepoteza simu yangu iliyokua na line mbili moja ya Vodacom nyingine ya Tigo, nikaonelea badala ya kuhangaika itafuta simu na polisi usumbufu kibao nirudishe tu namba zangu ili niendelee patikana hewani.
Kwenda Makao ya Tigo wakanambia niwaandikie namba tano zilizokua katika line yangu, nikaziandika pamoja na taarifa zingine na wakanisaidia ndani ya dakika 5 nikawa hewani tena!..kiukweli muda pekee nilioupoteza ni kukaa kwenye foleni kusubiri zamu yangu kuhudumiwa.
Baada ya kumalizana na ofisi za Tigo nikaenda ofisi za Vodacom hapo ndo usumbufu ulipoanzia.
Wakanipa fomu kujaza taarifa zangu kipengere cha kwanza tu wakataka namba 5 zilizokua zinanipigia mara kwa mara, mimi nikajua namba 5 zilizokuwepo ndani ya line!..
Nimekaa kwenye foleni kufika zamu yangu mhudum ananambia namba zimegoma tokea kwenye system yao yaani hazikua zinanipigia mara kwa mara!..Wakaniuliza imepotea lini line kuwaambia ni jana yake tu, wakashangaa yani walijua imepotea week (ina maana voda kurudisha line mpka kipindi kirefu kipite?).
Suluhu ya mwisho yure mhudumu kaniomba nisubiri mpaka siku kadhaa zipite lakini pia wakati nasubir nikumbuke namba zilizokua zinanipigia mara kwa mara!. Tatizo ile ya voda ilikua inatumika kutuma na kupokea fedha tu, haikua ya kupiga simu saana.
Mpaka sasa hivi sijafanikiwa kuirudisha ile line na mbaya zaidi ilikua na hela yangu, maana niliifanya kama benki yangu. Kwa ambaye amewahi kutana na tatizo hili alifanyaje kurudisha line?..