Vodacom na CRDB kuna mtandao wa wizi hatari

Vodacom na CRDB kuna mtandao wa wizi hatari

Kwa kifupi, kama kuna malipo ya bili mbalimbali au kuhamisha kutoka au kwenda bank, usitumie Mpesa. Ukinunua umeme leo unawezakupata baada ya wiki nzima kwenda bank ndio usiombe kabisa
 
Kwa kweli siwezi kuvumilia kwa hili,huu ni wizi wa kishenzi kabisa mnataka kunifanya na naapa nitawadhalilisha nyie watu na mtanilipa fidia kubwa sana,leo nimehamisha salio kidogo la pesa kutoka ktk akaunti yangu ya CRDB kwenda m pesa,nipo mbali na benk nikaona huduma hii itanifaa na nina shida hasa sina hata cent,cha ajabu tangu asubuhi hadi sasa pesa haijaingia kwenye m pesa yangu pamoja na CRDB kunitumia msg ya ref kuonyesha kuwa pesa imetumwa ktk m pesa na namba ya ref ninayo,kwenye akaunt yangu nimeangalia salio nikaona limepungua kwa kuhamishwa kwenda m pesa,sasa pesa zangu mmepeleka wapi nyie watu?

Mbona mnaonekana kabisa kuwa mmeniibia,nitawapeleka mahakamani nyote nidai fidia kwa usumbufu mlionipa, nitadai mamilioni ya fidia,mnajitangaza kwa gharama kubwa,kumbe hamna lolote utapeli tu umewajaa,mi nina shida bwana,pesa zangu ziko wapi? tangu asubuhi? nyie ni wezi mmepanga kunipiga kimya,nataka pesa zangu bwana mbona hamna hata aibu nyie mkoje lakini? NATAKA PESA ZANGU MIE NINA SHIDA HAPA NILIPO.

UPDATES
pole mkuu,hiyo huduma inakawaida ya kuchelewa kuhamisha fedha kutoka akaunti ya CRDB,kwenda M PESA,wakati mwingine inaweza kuchukua hata saa nzima,pole sana
 
Back
Top Bottom