PCGAMES
JF-Expert Member
- Apr 11, 2013
- 802
- 1,192
Naombeni mawazo yenu hasa kwa wale wenye uzoefu na mkoa wa Tabora. Mtandao upi ni mzuri zaidi kwa matumizi ya Internet kwa njia ya Modem kati ya Vodacom na Airtel na je, zote zina 3G huku Tabora? Nauliza ivyo kutokana na kujionea mwenyewe mtandao wa tigo kunigomea kutumia internet yenye kasi kama nilivyokuwa naitumia kipindi nilipokuwa Dar, na nilipokwenda ofisini kwao huku Tabora kuuliza kulikoni? Nikaambiwa tigo ya Tabora ina 2G kwa hiyo niwe mpole na nikubaliane na hali halisi ya mtandao wao. Sasa nina mpango wa kununua Modem nyingine hukuhuku Tabora maana kurudi Dar hadi majaaliwa. Sasa ninunue Modem ya Voda au Airtel maana ndizo zinazoonekana kuwa na nguvu zaidi huku Tabora. Ahsanteni.