hippocratessocrates
JF-Expert Member
- Jul 1, 2012
- 3,598
- 1,545
Salaam.
Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko karibu kila kona hasa kwa watumiaji wa mtandao huu(mimi nikiwa mmoja wapo). Pesa(Salio) kupungua kila wakati tena ukiwa hujafanya matumizi yoyote ya kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi au kutumia intanet i(off mobile data connection).
Binafsi nimekuwa mhanga wa tatizo hili kwa maana ilifika hatua matumizi yanakimbilia sabini elfu(70,000/=Tshs) kwa mwezi. Nimetafuta msaada bila mafanikio, tatizo hili lilishawahi kunitokea mwaka huu mwanzoni, nimeshazunguka sana Mlimani City (HQ) kwani nilidhani shida ni katika 'line' au simu yangu tu.
Majibu ya wafanyakazi/watumishi wao wa kitengo cha huduma kwa wateja hayaridhishi na wakati fulani yanakatisha tamaa.
Hapa jamvini, watu wameshalalamika sana na hata 'Sticky thread' kuanzishwa lakini hakuna mabadiliko. Hakuna msaada hata kwa member ajiitaye Vodacom Tanzania.
Sasa leo tena vifurushi kubadilika tena,kila siku wana jipya, na jipya lao ni bovu kuliko lililopita. Hapa sasa 'nimeomba poo'.