VodaCom mna vifurushi ghali mno, mtafukuza wateja wengi sana

Johnny Sins

JF-Expert Member
Nov 4, 2019
2,538
3,826
Yaani hata kifurushi cha 500 cha kueleweka hanma?

Yaani hata kile cha DAR UNI Tsh 500 mnatupa midakika kibao na miSMS nyomi na viMB 5 siriazi kweli?

Bora nirudi zangu nyumbani TTCL kumenoga.
 
Kuna wadau hawaangalii gharama za vifurushi wanaangalia ubora wa huduma. kuna mitandao mingine wanakupa 500mb kwa 500/=tsh alafu speed mbovu.

Ukimpigia mtu wala hamsikilizani au unaambiwa namba haipatikani wakati unaempigia yupo hewani,kufanya miamala pia ni mbinde kila siku mtandao unasumbua.
 
Tumeingia uchumi wa kati sasa, so vifurushi vitakuwepo kuendana na hadhi ya kati.
Haya mambo ya kupanda kwa uchumi yanaenda sambamba na huduma kama hizi kuongezeka ubora ila bei inapungua sio kuongezeka.Na watu wengi kupata access ya net.
 
Back
Top Bottom