Vodacom kusukuma gurudumu la elimu bure

Sudysoko

JF-Expert Member
Aug 19, 2015
449
180
Makubaliano yaliyofikiwa kati ya Wizara ya Elimu na kampuni ya IBM katika kusukuma Elimu Kwa njia ya dijitali huenda yakaafikiwa baada ya kampuni ya vodacom kufanya uwekezaji katika kusambaza miundombinu yake ya Minara Kwa kurahisisha huduma wa upatikanaji wa Intanenti.

Kampuni hiyo ndiyo inayoongoza katika sekta ya mawasiliano za simu za mkononi nchini kupitia sera yake ya kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali na kuyabadilisha maisha ya watanzania kupitia teknolojia.

Kampuni hiyo kwasasa inawafikia asilimia 88 ya watanzania ambao wananufaika Moja Kwa moja kwa huduma ya mtandao wa Vodacom kutoka katika minara zaidi 2700 ya huduma ya 2G, Minara 2000 ya 3G pamoja na Minara 278 ya 4G kwa Dar es Salaam, Kila mwezi vodacom Tanzania inatoa huduma ya data nyingi zaidi ya Petabytes 2 kulinganisha na mitandao mingine kutoka na uhitaji na idadi ya watumiaji wake kwa kadiri Intaneti inavyozidi kuongezeka na kusambazwa kutokana kuwepo kwa idadi kubwa ya miundombinu ya minara yenye kutoa huduma nchini.

Hali hii ya usambazwaji wa Minara itasaidia kufikia malengo ya Wizara ya Elimu kuwaunganisha watanzania pamoja na kutoa Fursa kupitia uwezeshaji wa Elimu pamoja kuwawezesha walimu na wanafunzi kufaidika kutumia huduma za dijitali katika kujifunza na kubadilishana mawazo.

Aidha hii ni nafasi ya watanzania kufaidika kwenye sehemu ya Gurudumu hili la kuwezesha Elimu bure kwa kununua hisa za Vodacom kulingana na huduma na uwekezaji katika kampuni ya Vodacom Tanzania.
[HASHTAG]#WekezaNaVodacom[/HASHTAG] Tanzania..

wanafunzi.JPG
wanafunziiii.jpg
 
Back
Top Bottom