Mkuu, pengine mimi nilipaswa kuanzisha thread mpya juu ya wizi wa namna hii kwa TRA kitengo cha road licence lakini kwasababu aina ya wizi vinafanana niwatonye tu kuwa hata TRA kuna wizi kama huu wa voda. TRA wanachofanya, ukienda kulipia road licence, kiasi kile unacholipa benki sicho hicho unachoandikiwa kwenye risiti unayopewa wakati unachukua stika. Mimi nililipa sh.180,000 lkn siku naenda kuchukua road licence yangu wakawa wameniandikia sh.120,000 na gari yangu wameishusha cc kama ya bajaji, Mungu wangu! Nilihoji kwanini imekuwa hivo lkn afisa anayehusika alionekana kubabaika na kuniambia ni bahati mbaya imetokea labda abadili aandike kwa mkono. Nikamuuliza kama kuandika kwa mkono ni utaratibu akachanganyikiwa zaidi.
Nipo safari nikirudi nitaangalia kama nitaweza kufuatilia maana inaweza kula muda wangu na huenda ni genge kubwa ambalo hata wakubwa wamo nikaishia kuingia gharama zaidi. Naomba mtakaosoma hii thread mhakiki vizuri ile kopi inayobaki unapokata road licence ili uone kama pesa ulolipa ndo iloandikwa hapo maana pia huandikwa kwa maandishi madogo sana.
Mimi walikwapua 60k, wakifanya hivyo kwa watu 100 kwa siku halafu kwa mwezi ni hela ndefu sana halafu tunashangaa mahekalu yanayoota kama uyoga kila siku. Hii ndo Bongo; I love my country!