Vodacom inawaibia wateja, serikali fanyia kazi

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
3,741
6,430
Ndugu watanzania,

Nimeshuhudia Vodacom inawaibia wateja pesa zao za muda wa maongezi kwa namna ifuatayo.

Mimi huwa ninanunua mda wa maongezi kwa ajili ya matumizi ya mda mrefu ili kupunguza buguza za bajeti. Hivyo huwa ninaweka mda wa maongezi wa laki na nusu angalau nitumie kwa miezi mitano.

Cha ajabu baada ya mudafulani ninapata messeji inasema mda wako wa sh 50,000 u 70,000 umeishamda wake na hivyo kupunguziwa salio.

Najiuliza ni dhambi ipi mtu anakuwa amefanya hadi uninyang'anye akiba yangu ya maongezi wakati nililipa pesa kwa kampuni wakati ninanunua mda wa maongezi.

Je haturuhusiwi kununua mda wa maongezi kwa wingi harafu nikawa ninatumia kidogokidogo kadili ninavyotaka?

Ukweli kwa hili nahitimisha voda ni wezi wakubwa na ninaomba serikali iafnyie uchunguzi.
 
Serikali hii itakachoangalia ni je wamelipa kodi basi, Uwe unaweka hela yako kwenye Mpesa halafu unanunua vifurushi vya maongezi kwa gharama nafuu vya mwezi mmojammoja
 
Hayo makampuni ya Simu ni Cartels hatari sana, Sijui kwa nini serikali isiongeze Scrutiny kwa hayo makampuni!
 
Ndugu watanzania,

Nimeshuhudia Vodacom inawaibia wateja pesa zao za muda wa maongezi kwa namna ifuatayo.

Mimi huwa ninanunua mda wa maongezi kwa ajili ya matumizi ya mda mrefu ili kupunguza buguza za bajeti. Hivyo huwa ninaweka mda wa maongezi wa laki na nusu angalau nitumie kwa miezi mitano.

Cha ajabu baada ya mudafulani ninapata messeji inasema mda wako wa sh 50,000 u 70,000 umeishamda wake na hivyo kupunguziwa salio.

Najiuliza ni dhambi ipi mtu anakuwa amefanya hadi uninyang'anye akiba yangu ya maongezi wakati nililipa pesa kwa kampuni wakati ninanunua mda wa maongezi.

Je haturuhusiwi kununua mda wa maongezi kwa wingi harafu nikawa ninatumia kidogokidogo kadili ninavyotaka?

Ukweli kwa hili nahitimisha voda ni wezi wakubwa na ninaomba serikali iafnyie uchunguzi.
Mimi kuanzia leo nimeludi nyumbani tayari kwenye Tigo yangu nataka nayo nikaiweke 4G mambo yangu yatulie nimewashindwa Voda kabisa jamani
 
Serikali hii itakachoangalia ni je wamelipa kodi basi, Uwe unaweka hela yako kwenye Mpesa halafu unanunua vifurushi vya maongezi kwa gharama nafuu vya mwezi mmojammoja

VODA LAZIMA WAJITOKEZE NAKUELEZA KWANINI WANAFANYA HIVI.MIE MESSAGE ZAO NINAZO NI KWAKWELI TH 3 NITAKWENDA TACRA KULALAMIKA. HAIKUBALIKI NINUNUE MDA WA MAONGEZI NAKWA KUWALIPA PESA HALAFU WANIKATE KISA SIJAZIMALIZA KUZITUMIA PESA ZANGU.VODA KWA HILI BADO NASISITIZA NI WEZI. WAADISHI WA HABARI NAONMBA MWAHOJI VODA KWANINI WANAWAIBIA WATANZANIA?MBONA UMEME UKINUNUA UNITI NYINGI UNAKAA MDA MREFU UKITUMIA NA WALA HAWAJALAZIMISHA UZITUMIE UNIT ZOTE NDANI YA MDA FULANI
 
Yani hawa voda ni hatari hasa kwenye ivi vifurushi yani unapiga kidogo muda umeisha hii nchi viongozi wako kimya haki ya Nani najuta kuzaliwa Tanzania
 
Kuhusu wizi wa mitandao ni donda sugu!! Kwani ndani ya hiyo mitandao kuna mikono ya vigogo wa serikali,, kwa hiyo serikali haiwezi kulishikia bango suala hilo kwani ndani yake kuna maslahi yao.
 
Si wanakula na wakubwa.
Hili tatizo halitaisha kamwe,voda wataendelea na unyang'anyi mpaka tutakapokuja kupata rais anaejali hasa matatizo ya wananchi wake ndo ataweza kulimaliza hili
 
voda nimeamua kuwanyoosha kwenye data bado kwenye calls, nyambafu sana
 
Juzijuzi nimenunua kifurushi cha 2500 cha wiki nashangaa hata wiki haijaisha eti mda wa maongezi umeisha na wakati nikipiga mahesabu ya dakika nlizotumia kuongea hata nusu saa haifiki,yani ni kama wamehamishia kodi kwa watumiaji wa mwisho huku wakiendelea kupata faida ileile bila effect yoyote.
 
Kiukweli Voda hata mimi siwaelewi, juzi juzi nlikutana na dada mmoja analalamika kanunua kifurushi cha 1000 lakini cha kushangaza baada ya kuunga aliongea tu kidogo, kuja kupiga tena anaambiwa hana dakika! nilipoona huu uzi nikasema subiri nichungulie ndani, kumbe alichokuwa analalamika yule dada ni kweli! Vodacom siku hizi ukiwa umebakiwa na 15 kwenye akaunti yako huwa hata haikubali kubip kwenda mitandao mingine....
 
WAKUU NI KWELI WANATUIBIA KWA NAMNA MBALIMBALI.UKINUNUA BANDO KILA UPIGAPO SIMU UKIANGALIA MUDA ULIOTUMIA WEWE NA UJUMBE KUTOKA KWAO UTAONA WANAONGEZA SEK 2 MFANO UMEONGEA KWA SEK 69 WAO WANAKUAMBIA UMETUMIA SEK 71.HIKI NI NINI?
 
tatizo la wizi wa muda wa maongezi limekithiri voda na tigo.na hata uwape facts zote hawakurudishii ng'o.
fikiria kama kampuni ya simu ina wateja milioni 2 wakiamua kumuibia kila mteja sh 100 tu kwa siku wanajipatia sh milioni 200 ambazo wala hazipitii kwenye system ya TRA. halafu tunaambiwa mahakama ya mafisadi imekosa kesi.
TANZANIA BWANA,DU!
 
Ukinunua vocha ya elf 10 mfano unapewa DK 200 voda-voda na DK 20 mitandao mingine, cha ajabu hata ukipiga mtandao wa voda wanazitumia kwanza hizo dk20 za mitandao mingine ukija kupiga mitandao mingine unaambiwa huna salio, huo nao ni utapeli kama utapeli mwingine.
 
Back
Top Bottom