Vocha ya Airtel ya Tshs 1000/- ....... !!!

ukiwa na coin unakwangua lightly, sio utumie miguvu mpaka jasho linakutoka. Si kwa airtell tu bali mitandao yote

Sawa sijakataa.. Ila.. Kuna kitu kinaitwa malalamiko baada ya kuathirika.. Mi nimeanza kutumia simu ya mkononi tangu 2000. Mambo ya vocha mpaka nalalamika,ni kwamba yamenikuta na mpaka napost uzi huu,ni baada ya kusikia wengine wameathirika,na kuona mwenzangu akinunua mara mbili vocha.

Kwa maana hiyo suala si kukwangua kwa nguvu,maana vocha haziuzwi benki ili tuseme tukwangue kwa nidhamu. Hivyo nguvu hutegemea na mazingira unayoweka vocha yako. Wengine wanakwangulia juu ya goti,kwenye dash board ya gari,wengine hugeuza simu zao na kukwangulia juu yake,wengine wanatumia mchanga,wengine wanakwangua huku wakitembea..
Na wasipate matatizo yeyote na vocha nyingine isipokuwa za Airtel,tena za buku...

Anyway,ni mojawapo ya maoni...
 
Pole sana, ila kwa kuwa sasa umeshalijua tatizo, chukuwa tahadhari au mwachie anayekuuzia aikwangue kisha akusomee namba tu.

Asante kwa ushauri... Nami ndiyo hatua niliyochukua jana..
 
Mkuu Myamahodzo... Afadhali umenielewa na ni bahati kuwa wewe mwenyewe ni shuhuda wa tukio hilo. Tena ushuhuda wako ni kama vile umejibu hoja zangu na za waathirika wengine..

Kuhusu tabia za watu humu JF,ni kweli kuna watu wana matatizo hadi unashindwa kuelewa kama huko kuchangia nyuzi wamelazimishwa ama la...
 
Tuko pamoja mkuu!

Airtel wanatakiwa kuchukua hatua za haraka kwa hili.
 
hata mimi nimepata tatizo kama hilo.ukweli ni kwamba vocha za 1000 za airtel zina matatizo,me nimepata hasara ya 2000
 
hata mimi nimepata tatizo kama hilo.ukweli ni kwamba vocha za 1000 za airtel zina matatizo,me nimepata hasara ya 2000

Pole sana Sweet G... Ndiyo maana tunashirikishana mambo kama haya...
 
Mnyamahodzo,pole sana kwa tatizo lako na Airtel...
 
Pole sana, ila kwa kuwa sasa umeshalijua tatizo, chukuwa tahadhari au mwachie anayekuuzia aikwangue kisha akusomee namba tu.
niligundua kabla ya kukwangua kuwa imechubuka ! Nikaitema !
 
niligundua kabla ya kukwangua kuwa imechubuka ! Nikaitema !

Kutokana na maelezo ya mkuu Mnyamahodzo....
Airtel hawana mpango wowote wa kurekebisha tatizo lililopo,au walau kutusaidia kwa ile huduma ya customer care ili kuitambua na kumrudishia salio mteja kwa njia yeyote mbali na kwenda kwenye "ofisi zilizo karibu nasi"
 
Scratchly gently jamani hamuoni hiyo.Hasara zingine za kujitakia.
 
Mie pia iliwahi nipata hapa Nzega ati nikaambiwa niende ofisi yao iliyoko Mwanza. Ebu piga nauli kutoka Nzega hadi Mwanza! Naona hawa wako kibiashara zaidi wala si kutoa huduma. Poleee....!
 
imewahi nitokea pia nilikuwa naenda nchi jirani nikanunua vocha pale Namanga na ikawa hivo hivo kama vile imeloweshwa kwenye maji nikaitupa lakini vile vile ikajanitokea tena hapa hapa dar
 
hiyo ni kamali ya lazima, bila ridhaa ya kuingia, na ina wizi ndani.
 
Mie pia iliwahi nipata hapa Nzega ati nikaambiwa niende ofisi yao iliyoko Mwanza. Ebu piga nauli kutoka Nzega hadi Mwanza! Naona hawa wako kibiashara zaidi wala si kutoa huduma. Poleee....!

Yaani wanazingua sana wateja wao...
 
imewahi nitokea pia nilikuwa naenda nchi jirani nikanunua vocha pale Namanga na ikawa hivo hivo kama vile imeloweshwa kwenye maji nikaitupa lakini vile vile ikajanitokea tena hapa hapa dar

Tuko wengi yaani inabidi kama hii thread wanaisoma,wachukue hatua..
 
hiyo ni kamali ya lazima, bila ridhaa ya kuingia, na ina wizi ndani.

Nadhani Airtel tunao humu ndani kama wadhamini mojawapo wa JF..
Watakuwa wanasoma maoni yako..

Kiukweli ni kilio cha wengi...
 
hili nph tatizo.ninavocha ya airteltoka mwaka jana mwishoni.imeharibika nambana bado sijapata msaada
 
hili nph tatizo.ninavocha ya airteltoka mwaka jana mwishoni.imeharibika nambana bado sijapata msaada

Kuna mkuu hapo Mnyamahodzo..
Yeye ana majibu ya maswali yako.. Ila kwa ufupi,hawa jamaa hawajali wateja wao in terms ya unnecessary cash utilization to their customers..
 
Vocha za airtel za 1000 ni nyepesi kuharibika, mi mwenyewe hapo majuzi nlikwangua ikaharibika, nikapiga huduma kwa wateja wakanambia niende kwa mawakala ndo wanisaidie. Wakati swala ni kutaja serial number mchezo unaisha. Sidhani kama hawa jamaa wanatujali wateja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…