Vizuri kujua kipaji chako

my name is my name

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
2,016
2,397
Kila mtu duniani ana kipaji chake. Utaangaika lakini ipo siku kipaji chako ndo kitakusaidia. Je wewe unajua kipaji chako? Umefanya nini kutambua kipaji chako? Unafanya nini kipaji chako kiwe bora kila siku? Kipaji chako kimekusaidia nini?
 
Lbda ungeorodhesha list ya vipaji hapa thn tukajitahmini km tuna moja kati ivo vipaji au lah...maana unaweza kuwa na uwezo flani lkn ucjue kuwa ndo kipaji chenyewe icho.
 
Inasemekana nje ya kipaji chako hauna nguvu ya ziada kwasababu sio kitu chako lkn ukifanya mambo kulingana na kipaji chako ndo dunia lazma ukutambue lkn pia watu wachache huwa wanabahatika kutambua kipaji chao hii kutokana na aina ya maisha tunayoishi hatujajipa kipaumbele sana kuishi na kufanyia kazi talents zetu aidha elimu ama ugumu wa maisha...
 
Mfano mm kipaji changu ni mzuri wa kupanga mipango na nikahakikisha naitekeleza na ni mtu creative najua kuona fursa na kuifanya kwa namna yapekee hata wengine walishindwa mm nita cone up na mbinu ingine kabisa namshkuru sana mungu kwa kuniumba hivyo na pia namshkuru kunjfungua mapema nategemea kufanya mengi makubwa siku za usoni mnaezakuta maneongea na billionaire la tz lijalo bila kujua
 
Mimi nina kipaji cha kunywa bia, nikipata pesa lazima ninywe mpaka ziishe sometimes nasahau hata kubakiza nauli ya bajaj inabidi niwaimbishe makonda.
 
Mimi bado kuna jambo linanipa maswali kuhusu hivi 'vipaji'....

Hivi mtu kama MJ alikuwa bonge la super star ulimwenguni, lakini MJ na ndugu zake walipozaliwa walimkuta Baba yao tayari ni Mwanamuziki, nao ndio wakafanya muendelezo na kupelekea MJ kuwa MJ...... sasa je, kile ndio kipaji ama? na je kama MJ angezaliwa kule Namtumbo Ruvuma bado angekuwa MJ yule mwenye kipaji kile?

Mwingine ni Serena Williams...Yeye na dada yake Venus walikuta Baba ni mwalimu wa tennis,nao wakaanzia hapo, leo hii dada hao ni gumzo ulimwenguni...sasa je nao wana vipaji? na kama wangezaliwa kule Kazuramimba, bado wangekuwa na vipaji vya kucheza Tennis?

Mimi kuna wakati huwa nafikiri kwamba mtu kama MJ hata kama angekuwa Dokta basi angekuwa mwenye uwezo wa kipekee, au kama angekuwa Mwanariadha basi angekuwa mithili ya Usain Bolt , kwenye soccer angekuwa Pele n.k n.k.
 
Mfano mm kipaji changu ni mzuri wa kupanga mipango na nikahakikisha naitekeleza na ni mtu creative najua kuona fursa na kuifanya kwa namna yapekee hata wengine walishindwa mm nita cone up na mbinu ingine kabisa namshkuru sana mungu kwa kuniumba hivyo na pia namshkuru kunjfungua mapema nategemea kufanya mengi makubwa siku za usoni mnaezakuta maneongea na billionaire la tz lijalo bila kujua
Hongera sana aisee Mungu akuongoze ukapate kufanikiwa, wengine hapa hata vipaji vyetu hatuvijui.
 
Back
Top Bottom