#COVID19 Viwapi virus vya SA, UK & Brazil

KISIWAGA

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
8,024
16,490
Wadau,

Kama mnavyokumbuka kuna kipindi viliibuka aina mpya za virusi vya korona vya kutoka South Africa, Brazil and UK.

Virus hivi hasa kile cha SA vilisemekana kuwa hatali zaidi na kuna baadhi ya nchi zilifikia hatua ya kisotisha safari zote kwenda SA

Muda umekwenda kwa sasa hatusikii chochote kuhusu hivyo virus na badala yake tunaletewa habari ya virus vipya vya kutoka India.

Swali langu la msingi ni je hiki kirus cha delta toka India ndicho kirus cha mwisho hatari ama labda baadaye kitakuja kingine na hiki cha delta kipigwe bench na wenye Dunia yao

Nidiclare interest kwamba mimi toka October mwaka Jana sichukui tahadhari yoyote dhidi ya korona na endapo hiki kirus cha delta kitapotea kwa style ile ile ya SA,BRAZIL & UK nitatangaza rasmi kuwa hakuna ugonjwa unaoitwa korona
 
Hivi hakuna hata anaevikumbuka,mbona naona kama vile tunapigwa kikondoo
Hivi vilikua haviko effective kwenye kutimiza lengo ndio maana wakaachana navyo wakaja na "version" mpya ambayo ndio inatupeleka mpela mpela kwa sasa. Lengo kuu ofcoz ni kupiga hela kupitia ujangili-tiba.
 
Wadau,
Kama mnavyokumbuka kuna kipindi viliibuka aina mpya za virusi vya korona vya kutoka South Africa,Brazil and UK.

Virus hivi hasa kile cha SA vilisemekana kuwa hatali zaidi na kuna baadhi ya nchi zilifikia hatua ya kisotisha safari zote kwenda SA

Muda umekwenda kwa sasa hatusikii chochote kuhusu hivyo virus na badala yake tunaletewa habari ya virus vipya vya kutoka India.

Swali langu la msingi ni he hiki kirus cha delta toka India ndicho kirus cha mwisho hatari ama labda baadaye kitakuja kingine na hiki cha delta kipigwe bench na wenye Dunia yao

Mkuu hii ngoma si ya akina babu wa Loliondo. Hii inakwenda mithili ya mawimbi ya bahari. Moja baada ya jingine. Kila linalokuja ni kali zaidi kuliko lililopita.

Ukiwa zuzu unaweza hata kudhani ugonjwa umeufukuza kwa maombi kumbe wimbi limepita tu.

Hayo yote uliyotaja, wenyewe wayaita hivi:

Alpha, Beta, Gamma, Epsilon, Delta, na bado.

Kama hatutashiriki kuuvunja mwendelezo huo, hili gonjwa bado tunalo sana labda hadi tutakapoungana prematurely na yule mwamba aliyekomaa nalo prematurely hadi dakika ya mwisho.

Sote hatuwezi kuelewa kila kitu. Hiyo ni kawaida. Mengine tuwaachie wenye taaluma zao. Short of that jipange kujiunga MUHAS kama fresher. Ubobezi wa hapa ni kwa kukomaa darasani si kwa kuoteshwa ndoto za nyungu, mikaratusi au matango pori.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Back
Top Bottom