maroon7
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 11,341
- 15,829
Wakuu, siku zote nilikua natamani sana kupata kiwanja maeneo ya milimani na nilikua napenda sana kutembelea maeneo hayo, sasa juzi kama bahati nikawa napiga stori na babu anayelinda sehemu tunapopark magari ndio nikajua naye kumbe ni kama fisadi maana anamaeneo makubwa mno ambayo yalikua mapori tu na aliamia miaka mingi na kuanza kuyalima,ikabidi anipeleke kuangalia maeneo yake na hakika nilistaajabu kukuta babu anamaeneo makubwa na mazuri vile na kumbe ndipo anapokaa maana tulifika hadi kwake ambapo ni mlimani pia(Na hakika nilijifunza usimdharau mtu usiyemjua maana washkaji tunaopaki nao magari hapo nao hawakuamini kuskia babu anamaeneo makubwa kiasi kile). Jirani na eneo lake kuna maeneo mengine yalikua yanauzwa yakawa yamebaki mawili mojawapo ni la mlimani ambako ndio hasa nilikua nayatamani siku zote. Sasa nataka ushauri kwa wanaojua sheria za hifahi ni mita ngapi labda mtu unatakiwa ujenge mbali na mlima maana nimeshaamua lile eneo siliachi na kesho nataka nikawaone wahusika akiwemo balozi wa eneo hilo kwa ajili ya ununuzi.
Hii ni picha ya eneo nililolipenda linalouzwa ambalo litatimiza ndoto yangu
Hii ni picha ya eneo nililolipenda linalouzwa ambalo litatimiza ndoto yangu