Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,502
- 22,355
Kiwanda cha Illovo Sugar ambacho kipo Tanzania kwa ajili ya kuzalisha sukari bora kwa ajili ya masoko ya Ulaya na Marekani inabidi kiangalie upya mikakati yake ya masoko.
Kiwanda hiki kikiweza kusambaza sukari kwa soko la Tanzania kabla ya kusafirisha kwenda nje hii itaokoa viwanda vyote vitano vya sukari ambavyo Tanzania inavyo na kutakuwa hakuna haja ya kuagiza sukari kutoka nje.
Kwa mujibu wa tovuti ya Illovo Sugar ni kwamba kiwanda hiki ambacho ni sehemu ya kiwanda kikubwa cha Kilombero Sugar pamoja na viwanda vingine vitatu wanazalisha watani wa tani 300,000 za sukari kwa mwaka.Hii sukari inatoka katika viwanda vyake vya Msolwa na Ruembe.
Tanzania ina viwanda vitano vya kutengeneza sukari na viwanda hivi ni Mtibwa Sugar, Kilombero Sugar, Kagera Sugar na TPC Ltd.
Katika hivi viwanda viwili Mtibwa na Kagera vinamilikiwa na mtu mmoja na Kilombero kuna viwanda viwili Illovo na Msolwa.
Illovo inamiliki asilimia 55 ya kiwanda cha Kilombero, na asilimia 20 inamilikiwa na kiwanda cha EDF & Man ambao ni Wazungu wa Uingereza.
Serikali ya Tanzania inamiliki asilimia 25 tu ya mtaji wa kuendesha kiwanda hiki yaani Share Capital.
Sasa linapokuja suala la uzalishaji na masoko ya sukari hii, ni moja kwa moja utaona kwamba kiwanda kama cha Kilombero kinazalisha tani zisizopungua 100,000 na hii ni kutoka katika taarifa zao na kwamba wana masoko maalum ya kuuza sukari hiyo ambayo inatoka Tanzania.
Lakini pia katika kuonyesha ukosefu wa umakini katika taarifa zake, bodi ya sukari wao katika taarifa zao wanasema kwamba viwanda vyote vya sukari nchini vinazalisha tani 300,000 kwa mwaka na kwamba mahitaji ya sukari kwa mwaka ni tani 590,000, ambapo tani 420,000 ni kwa matumizi ya walaji na tani 170,000 ni kwa matumizi ya viwandani.
Kiwanda cha Mtibwa Sugar kinazalisha tani 35,000 kwa mwaka na Kagera Sugar kinazalisha tani 40,000 pia kwa mwaka. Kilombero tani 80,000 na TPC Moshi tani 100,000 kwa mwaka.
KUNA HAJA YA SERIKALI KUWATUMA WATAALAM WAKE AMBAO NI SEHEMU YA ILE TASK FORCE YA RAISI, KUCHUNGUZA MAKARATASI YOTE YA UZALISHAJI NA MAUZO YA SUKARI NCHINI NA NJE YA TANZANIA KWA VIWANDA VYOTE VYA SUKARI.
Mpaka hivi sasa bodi ya sukari haijapata uwezo wa kutambua ni kwa kiasi gani kunahitajika sukari nchini, na pia bodi hiyo haina mbinu maalum za kupata taarifa za masoko, mahitaji na mauzo bila kusahau matumizi ya sukari kwa walaji na yale ya viwandani.
Ni wakati sasa umefika kwa serikali ya awamu ya tano kuendelea na kasi yake kwa kuangalia mkataba wa umiliki wa hisa zake 25 kwenye kiwanda hiki cha Illovo ili kuona uwezekano wa kuzinunua hiza hizo au kurudi mezani na wamiliki wa Kilombero Sugar ili kuwa na hisa sawa au kuzinunua zote kabisa.
Isitoshe Bodi ya sukari inabidi ivunjwe na mwenyekiti wake ajibu maswali kwanini bado haijatumia uwezo wake kudhibiti soko la sukari nchini hali ilopelekea kuwepo na matatizo ya wananchi kukosa bidhaa hiyo muhimu.
Angalizo:
Kabla ya kuja na kuanza kutoa mapovu nawaomba wanabodi kutembelea tovuti za Illovo Sugar na Sugar Board of Tanzania ili kupata picha halisi na unapokuja na hoja basi unakuwa umeelewa "the whole concept".
Home
Illovo Sugar