GE2025 Viwanda vipya 718 vimejengwa Geita

GE2025 Viwanda vipya 718 vimejengwa Geita

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,447
Reaction score
2,094
Rais Samia Suluhu Hassan, amejenga viwanda vipya zaidi ya 700 ikiwemo GGR kinachosafisha kilogram 440 za dhahabu kwa siku ajira mpya zaidi ya 14,000 zimezalishwa ndani ya miaka 4 ya uongozi wake

Katika kipindi hicho, viwanda mkaoni Geita vimeongezeka kutoka 824 mwaka 2021 hadi viwanda 1,542 mwaka 2025, hata hivyo ajira za viwandani nazo zimeongezeka kutoka ajira 927 mwaka 2021 hadi ajira 15,161 mwaka 2025.

Utoaji wa leseni kwa wafanyabiashara imeongezeka pia kutoka leseni 1,346 mwaka 2021 hadi leseni 2,815 mwaka 2025

Mfano wa viwanda hivyo ni Kiwanda cha kusafisha dhahabu cha Geita Gold Refinery (GGR) kimezinduliwa mwaka 2021 kikiwa na uwezo wa kusafisha hadi kilo 440 za dhahabu kwa siku na ni mojawapo ya viwanda vikubwa vya madini nchini Tanzania

Kingine ni Kiwanda cha kutengeneza baruti cha GGM kimeendelea kufanya kazi sambamba na viwanda vidogo vya vifaa vya ujenzi (tofali, nondo, kokoto) na viwanda vya kuchakata mbao

Pia kuna Viwanda vya kubangua pamba pia vimeongezeka kutoka 2 mwaka 2021 hadi 5 mwaka 2025, ikiwa ni juhudi za kuongeza thamani kwa zao hilo

Maeneo ya viwanda (industrial areas) yametengwa katika Halmashauri zote 6 ambapo Geita TC na Chato tayari yameanza kazi

000.png


Chanzo: ITV DIGITAL
 
Back
Top Bottom