Viwanda 3,500 vyaanzishwa nchini ndani ya miaka mitatu

Viwanda 3,500 vyaanzishwa nchini ndani ya miaka mitatu

mamayoyo1

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2018
Posts
1,011
Reaction score
1,019


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhandisi Stella Manyanya amesema jumla ya viwanda 3,504 vimeanzishwa nchini na serikali ili kujenga uchumi wa viwanda.

Amebanishha hayo Bungeni alipokuwa akijibu swali la mbunge wa Chumbageni, Ussi Salum aliyetaka kujua viwanda vingapi vimeanzishwa tangu Serikali ya Awamu ya Tano ianze utekelezaji wa mpango wa kuimarisha uchumi wa kati wa viwanda.


“Kati ya viwanda hivyo 3,504 vilivyoanzishwa, vinajumuisha viwanda vidogo sana 2,500, viwanda vidogo 943, viwanda vya kati 51 na viwanda vikubwa 10,” alisema.

Mhandisi Manyanya alisema wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina imekuwa ikifanya tathmini ya viwanda 156 vilivyobinafsishwa na kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukuliwa kwa viwanda 68 ambavyo havijaendelezwa.
 
Naomba kukuuliza mleta mada,hivi viwanda vilivyoanzisha vinafanya kazi/uzalishaji wowote,??na vimetoa ajira ngapi mpaka sasa(takwimu inasemaje juu ya hili)?!
 
ili tuendelee tunahitaji
watu, ardh na siasa safi... watu wapo, ardh ipo, siasa safi hakuna!
viwanda vitazalisha nini? malighafi je?
tumeshindwa kuzibangua kwa menoo tutaweza kwa viwanda?
 
Hapo sidhani kama na hiki kiwanda changu cha kusindika ice cream za ubuyu kimejumuishwa.
 
ccm inachekesha sana. Hata vile vimashine vya kukamua miwa vinaitwa viwanda, hata aibu hawana!! Naomba wataje mahala vilipo waache usanii wa mabundi
 
Serikali Ya Awamu Hii Ya Tano Ni Viwanda
Ndugu Zangu Mniamini Niwafanyizie Kazi
 
Hi kaulimbiyu imekufa kifo kibaya sana.
 
Magufuli akubali kuusikia ukweli mchungu,

Tanzania hatuna viwanda hata 100 vyenye hadhi ya kuitwa viwanda kwenye nchi za wengine,

Suala la viwanda limechanganywa na siasa zaid badala ya uhalisia,

Magufuli amependa kusikia idadi za viwanda vikitajwa bila kufanya upembuzi yakinifu na kujua hasa ni viwanda gani anatajiwa?

Tunataka kujua viwanda vya machine ni vingapi

Vya Nondo na material muhimu ya kujengea ni vingapi

Vya baiskeli ni vingapi,

Vya simu ni vingapi

Vya redio ni vingapi

Vya piki piki ni vingapi

Vya viatu ni vingapi

Vya magari ni vingapi

Tusihesabu cherehani na vibanda vya kusindika juice

Britanicca
 
viwanda hapo ni 10 tu
Ili kuhalalisha tume categorise viwanda katika nyanja 4:-
1.Viwanda vidogo sana (sindano, wembe, kisu, chanuo nk). Sindano inatumika na kinamama wanaofuma mashuka na vitambaa vya mezani. Wembe kwa wanaonyoa kwenye salon za vihijini. Kisu ni kiwanda kwa wanaouza matunda Stendi mfano machungwa, maembe nk. Chanuo ni kiwanda kwa kinamama wasusi.
2.Viwanda vidogo (Panga, Jembe la mkono, Sululu, nk)
3.Viwanda vya kati (Vyerahani, mashine za kubangua karanga, mashine za kupukuchua mahindi nk)
4.Viwanda vikubwa (Viwanda vya maji, saruji, Unga, tambi, nk)

Sasa wewe endelea na ubishi wako utaitwa beberu muda si mrefu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona 3500 ni kidogo angesema viwanda 350000000
 
Back
Top Bottom