Vivuko vyote nchini vifungiwe weight sensor

Vivuko vyote nchini vifungiwe weight sensor

kindikwili

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2016
Posts
1,862
Reaction score
2,876
Kwanza napenda kuwapa pole ndugu wote waliopatwa na msiba huu mzito pamoja na watanzania kwa ujumla.

Napenda kutoa mapendekezo kwa serikali kuhusu namna bora ya kuhakikisha kuwa vivuko vyetu havipakii kuzidi kiwango kinachoruhusiwa. Pendekezo langu ni kwamba vivuko vyote viwe na weight sensor and recorder. Yaani ubuniwe mfumo bila shaka mifumo hii ni mingi na kama haipo wapo vijana hapa nchini wanaweza kutengeneza, mfumo huo uwe na uwezo wa kurekodi na kuonesha uzito wa watu na mizigo kwenye vivuko vyetu. Mfano mkiingia tu kwenye kivuko na mizigo ikawekwa uzito wa watu na mizgo uoneshwe kwenye screen utakaofungwa kwenye kivuko baada ya kurekodiwa na mfumo husika. Kama uzito utazidi basi watu au mizigo au magari yapunguzwe kabla ya kivuko kuanza. Hii itasaidia sana na itaondoa usumbufu wa kutaka kujua uzito wa walioko kwenye kivuko kama ilivyo sasa.

Jambo la pili la kufanya ni kwamba life jackets na yale maboya yasiwe yanafungwa kwa kamba kwenye vivuko au kufungiwa kwenye chumba maalumu, kwasababu wakati wa ajali taharuki huwa kubwa na hakuna anaweza kukumbuka kwenda kufungua hicho chumba kilicho na maboya na life jackets . Nimekuwa abiria mzuri sana wa baadhi ya vivuko vyetu hasa kati ya magogoni na kigambani, kati ya mwanza na sengerema pamoja na mwanza na ukerewe lakini kote huko maboya na life jackets zimefungwa kwa kamba ngumu kwenye vivuko/meli na mengine kuwekwa kwenye chumba maalum. Wakati wa ajali yanakuwa useless. Pili mara kwa mara abiria wafundishwe namna ya kuyavaa

Laiti yale maboya na life jackets yangekuwa hayajafungwa au kufungiwa sehemu kwenye kivuko cha MV Julius , baada ya kivuko kupinduka yangezagaa juu ya maji na baadhi ya watu wangejiokoa na kupunguza idadi ya vifo.

Sitaki kumlaumu mtu japo kuna wakati naona wapo watu wanapaswa kulaumiwa sana, itoshe tu kusema ni heri kuziba ufa kuliko kusubiri kujenga ukuta na bora ukuta huwa ni matofali na cement hapa tunazungumzia uhai wa binadamu ambao ukitoka haurudi. Hili liwe funzo la mwisho kwetu

NB. Serikali ianzishe effective and efficient rescue team with all modern facilities katika maeno yote ya maziwa yetu kama Musoma, mwanza, ukerewe (kwa sababu maalum), bukoba, nyasa, etc.

Mungu ibariki Tanzania.
 
Kama watazingatia operational and safety measures za ku-operate vivuko/meli zinazotolewa na watengezenezaji hamna shida. Nasema hivi kwani haya yote uliyoelezea huwa yanazingatiwa wakati wa kutengezea vivuko/meli. Kwa mfano kitu kama meli. Usifikiri watengenezaji hawakuweka kipimo chochote kuonyesha uzito iliyobeba na kama imezidisha! Kuna kitu kinaitwa load lines. Kwa kifupi huonyesha uzito ambao meli imebeba na uzito ukizidi inajulikana! Kimbembe kinakuja chombo kinapokuwa chini ya himaya mwafrika mwenzangu! Hapo kila kitu anatupa kule na kuamua kufanya yake.
 
Kadhalika monitoring cctv cameras
 
Back
Top Bottom