Nilichungulia kupitia ule mwanya pale
dirishani
na kuona gari moja aina ya verosa ikiingia
pale hostel na robo saa baadae mpenzi wangu
Vivian akiwa na rafiki yake wa karibu Nancy
wakaingia katika lile gari na likaondoka.
Ilinuchukua zaidi ya saa kufikiri na baadae
nikafuta machozi ambayo yalianza
kuninyemelea
na nikaondoka zangu pale na kwenda zangu
mitaani nikiacha baaadhi ya mabinti
wankinong'ona kwa chinichini kuwa bila hela
huwezi miliki mtoto mzuri mjini.
Niliumia sana nikafikiri miaka miwili
tuliyokaa
pamoja na jinsi alivyokuwa akitumia fedha
zangu
na sasa eti kwa kuwa nimefulia ndio anaanza
kunidharau na kunidhalilisha hivi.. Na kama
vipi si angekuwa mkweli tukaachana?
Nikaanza kuona hasira zinanizidia na kila
siku
napunguza spidi ya darasani jambo amablo
hata wenzangu wakanishauri niachane nalo.
Kweli niliachana nalo ingawa kila nilipomwona
Vivian akiingia kwenye lile gari la yule
mzungu nikaumia sana.
Jumapili moja nikamwomba Nancy aniitie
Vivian na kuandaa sehemu moja nikae na
kuongea nae kwa masaa kadhaa ingawa neno
nililoambulia ni kuwa hajisikii tena kuwa na
mimi kwani hana tena mshipa wa upendo juu
yangu.
Nikamuuliza kama kuna sehemu nimekukosea
niambie kwani nimejitahidi kukupenda
atakavyo na tulipendana sana tukiwa na
ahadi zetu kibao lakini sasa hapa chuoni
kumegeuka kuwa na story moja tu ya mimi
na yeye kuachana na yeye akiwa na mme
mpya mwenye fedha.
Nikamwomba hata kama nimemkosea na
hatataka tuwe tena wapenzi basi tuwe tuu
marafiki na huyo jamaa kama inawezekana
awe anaonana naye huko nje akija hostel,
kwani
aondokapo pale hostel hugeuka na kuwa na
mada moja ya kuniponda mimi sasa inanipa
wakati mgumu.
Akaniangalia toka chini mpaka juu akadai
"usiniingilie katika mambo yangu, nitafanya
nitakavyo." Niliumia kwa kweli na kuanza
kufanya utaratibu wa kuhamia mtaani lakini
kabla ya kufikia mwisho nikamshirikisha
rafiki yangu mmoja.
Akaniambia nisiwe mjinga na kuamua
kushindwa
kijinga jinga, hivyo akaniambia kama nina
kitu
chochote ninacho cha kuweza kummwaribia
niseme... nikagoma kwani sikuona kama
ingekuwa na tija yoyote zaidi ya kuniletea
madhara.
Siku chache baadae rafiki yangu akaja na
wazo kuwa kwa nini tusimwaribie Vivian ili nae
aumie kama navyoumia mimi? Maana muda
mwingi nilikuwa mnyonge na ile hali ikawa
ikimfanya rafiki yangu kunichukia sana.
Wazo lake likawa ni kama mimi nilishawahi
kumpiga picha yoyote vivian akiwa uchi au
yeye kama anazo kwenye simu. Mimi
sikuwanazo kwa kuwa sikuwa napenda kukaa
na picha kama hizo kwenye simu au hata
kuthubutu kumpiga picha hizo.
Kilichobakia ikawa ni kumtumia rafiki yake
Nancy ambaye akaniambia kuwa picha zipo.
Nikamlipa hela na picha zile nikazihifadhi
nikisikilizia maelekezo ya rafiki yangu.
Rafiki yangu akaniambia sasa kitu cha
kwanza ni
kutengeneza akaunti feki ya facebook yenye
jina lake, na kisha kuziweka picha na baada
ya hapo zianze kusambaa kutoka kwenye
akaunti hiyo na kisha kwenda kwenye blogs,
whatsapp, na mitandao mingine ya kijamii.
Wazo lile nikalipenda kwaniwakati huo ubongo
wangu ulitaka kulipa kisasi tuu na kuona
Vivian akigalagala huku akilia kwa aibu kama
mtoto mdogo, akishindwa kula na hata
kuiona shule chungu na hata afukuzwe tu.
Mpango ukakamilika na harakati zikaanza
na ninakumbuka ilikuwa ni jumatatu moja
majira ya
saa nne nikaona mabinti pale hostel wakitoka
mbio kwenda nje..
Sikutaka kwenda maana sishabikihi umbea
lakini
kelele na mabishano yakazidi na nikaona
niende
maana kila mtu alikuwa akienda huko.
Kufika pale nikaona watu wamzunguka mtu
na nilipojaribu kupenyeza macho nikakuta ni
Vivian akiwa kaanguka na ana damu tumboni
zikimtoka na kabla ya kujua nini
kinaendelea ambulance ikaja na kumchukua
na baadhi ya watu wakamshindikiza.
Wazo la kwanza lililonijia nikajua lazima
damu zile zitakuwa zimesababishwa na ugomvi
kati ya Vivian na yule mzungu wake.
Nikajivuta mpaka chumbani kwangu ambako
nikaichukua simu yangu iliyokuwa kwenye
chaji na kumpigia rafiki yangu ili kumpa
mkanda mzima.
Tukafurahi na kukutana bar moja nje ya
hostel
na kupata bia zetu tukijua sasa dada ndio
moto
unamwanzia, labda mzungu kaona zile picha
maana zilishaanza kusambaa kwa kasi na
akaamua kumpa kipigo cha mbwa mwizi si
wajua waungu wengi wanapenda mieleka.
Wakati huo Nancy alikuwa akitokea hospitali
na alituona na kuja pale haraka huku
akihema na kusema "mmefanya nini
sasa,Vivian kapigiwa simu na baba yake na
baadhi ya ndugu kuwa wameona zile
picha ....kwani nyie mlimpa nani picha?"
Nikakumbuka kuwa Nancy tulimdanganya
kuwa zile picha nitakaa nazo mimi kwani
namkumbuka sana Vivian katika kipindi hiki
alichonisaliti.
Nancy akaendelea kuongea kuwa Vivian
kajichoma kisu cha tumboni ili afe kwani
ilikuwa ni aibu kupigiwa simu na ndugu zake
wakidai aache shule na arudi nyumbani
kwani ni badla ya kusoma anafanya kazi za
kikahaba.
"Na pia yeye kakuhisi wewe ndio umefanya
hivyo sasa sijui itakuaje wakijua na mimi
ndio nilitoa picha hizo??? yaani nimeishiwa
nguvu hapa shemeji", aliongeza maneno hayo
Nancy huku akifuta jasho na kuonyesha hali
ya kuwa na hofu.
Muda huo zile bia tano nilizoziweka kichwani
kwa furaha nikaziona zikiishia kichwani na
akilikuja. Nikamuuliza rafiki yangu kaka
tufanyeje maana sasa ushahidi unaonyesha
kuwa utaonekana au?
Akaniambia wala usijali tulitumia computer
ambayo sio yetu hivyo hatutashikwa sisi
hatawakifuatilia IP Adress. Tukiwa tumekaa
pale twajadiliana maratukasikia king'ora cha
gari bila kufikiri ni cha gari la polisi au
ambulance tulikimbia tukielekea nyuma ya
hosteli na kisha kutokomea mtaani.
Nikaanza kuona sasa kama ule uhuru wangu
wa mtaani ukinitoka na muda huo zikaanza
kuingia message kutoka kwa marafiki
zikisema, "kaka
umemuua Vivian kisa kusambaza picha zake
kwenye mitandao"......
Nikaizima simu hiyo na kuwasha simu yangu
yenye laini nyingine. Ilivyowaka tu ikaingia
sms
ya VIVIAN iliyotumwa masaa mawli nyuma
ikisema,
" NAKUSHUKURU KWANI NAJUA NI WEWE TU
ULIYEZITOA PICHA HIZO ILI MIMI
NIAIBIKE, NA
KAMA KUNA BAYA UNALIPANGA KWANGU BASI
LIKURUDIE..ASANTE"
Mungu wangu!!!! nikaona kama aliandika
hivyo basi ni ushahidi tosha wa kuniweka
hatiani. nikamwangalia rafiki yangu na
Nancy nikawa sina la kusema zaidi ya kulia.
Nancy akasema kuwa anakumbuka simu ziko
hostel hivyo tukawahi kwenda kuziangalia ili
pengine tufute ule ujumbe, tulifanikiwa
kuzikuta na tukafuta ule ujumbe na kisha
kufuta picha zote online na kuamini sasa
hakuna kesi.
Baadae tukaitwa kwenda ukumbi mkubwa na
kuambiwa ya kuwa Viviani alifariki muda
mfupi baada ya kupelekwa hosptitali
kutokana na kuvuja damu nyingi kwenye
jeraha. Na polisi wanaendelea kuchunguza
nini kimesababisha vivian kujiua.
Wiki moja baada ya mazishi walikuja jamaa
wawili na kunichukua mpaka kituo kikuu cha
polisi na kunifanyia mahojiano.. Nikiwa pale
nikaonyeshwa picha za VIVIAN na hata zile
meseji na moja kwa moja nikaonekana ni
mtuhumiwa namba moja.
Machozi yakaanza kunitoka na kujutia
uamuzi nilioufanya kwa shinikizo la rafiki
yangu na kuwa
sasa kesi yote ni yangu.
Nikapandishwa kizimbani na baada ya muda
mchache nikagundua kila ndugu na rafiki
wameniacha na kwa kuwa nilikuwa sina hata
ubavu wa kumweka wakili basi kesi ile
ikanikalia kooni.
Siku ya hukumu nikaambiwa kuwa
nitahukumiwa kunyongwa kwa kuchomwa
sindano yenye sumu. Siku ilipofika nikaletewa
mchungaji nikakaa nae na kutubu dhambi
zangu zote..
Nikaongea akanitia moyo kuwa kuna maisha
baada ya kifo na kuwa Mungu haangalii
mwanzo bali mwisho. Baada ya kunifanyia
maombezi nikamwambia kuwa, siku hiyo
ningependa kabla ya kuuawa nile Ugali na
dagaa
na kachumbali chakula nilichopendelea sana
kula nikiwa na Vivian. Nikaletewa ugali na
dagaa na soda moja ya kopo.
Baada ya kula nikawekwa kwenye kiti tayari
kwa kunyongwa. Sindano ya sumu ikawa
imeruhusiwa nikawa naona maumivu makali
sana na kwa mbali mkojo ukaanza kunitoka
kwa kasi kuashiria ya kuwa ndio nakata roho.
Baada ya dakika chache nilishtushwa na
kibao kutoka kwa mke wangu
kumbe nilikuwa naota.... nakojoa kitandani
usiku. Duuuh Ndoto kama hizi sizipendi..!!