Viva JF Viva love connect

Ntigy

JF-Expert Member
Mar 23, 2014
489
267
Awali ya yote namshukuru Mola muweza wa yote.

Pili naishukuru JF kwa kuanzisha jukwaa hili la LOVE CONNECT.

Bila shaka jukwaa hili limeunganisha wapenzi wengi,japo ni jukwaa ambalo baadhi ya wadau wamekuwa wakilikandia na kuwakatisha tamaa wanaotafuta wenza/wapenzi hapa.

Miezi kadhaa iliyopita nilijitokeza jukwaani hapa kutafuta mme mtarajiwa,kama ilivyoada wadau mbalimbali walicomment wawezavyo wapo waliokandia,lakini kuna walionitia moyo.

Nawashukuru wote waliochangia bila kujali kama walikandia au walinitia moyo,hii ni kwasababu walinipa hamasa ya kuendelea na mchakato wa kumsaka mme wangu mtarajiwa.

Zaidi ya yote nawashukuru wote walionitumia PM, na ninaomba msamaha kwa yeyote niliyemkwaza.

Namshukuru Mungu,amenikutanisha na mwanaume wa ndoto zangu kupitia JF,ni mwanaume mwenye sifa zote nilizotamani mme wangu mtarajiwa awe nazo.

That is why napaza sauti nikisema,

VIVA JF! VIVA LOVE CONNECT!
 
Mi naonaga kama maigizo haya eti sijui kwa nini

tehe tehe tehe tehe kuna waliovuma sasa ivi siwaoni,wengine wanarudi mbio tena hapa kuwaponda waliowapata ila maigizo haya ni mazuri coz huoni picha,picha unaitengeneza mwenyewe kichwani
 
Back
Top Bottom