Vituo vya utalii vijengwe nchini kote sio Dar tu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vituo vya utalii vijengwe nchini kote sio Dar tu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mallaba, Feb 17, 2011.

 1. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #1
  Feb 17, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  Vituo vya utalii kujengwa Dar

  HALMASHAURI za Jiji la Dar es Salaam, zimeshauriwa kutenga maeneo kwa ajili ya kujenga vituo vya kitalii ili ziweze kujiongezea mapato.

  Ushauri huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Emmanuel Ole Naiko, kwenye kikao cha mashauriano kilichofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

  Ole Naiko alisema lengo la kikao hicho ni kuhakikisha kila wilaya inaainisha maeneo yake, ili atakapopatikana mwekezeji ajenge kituo cha kitalii kitakachosaidia kufanya Dar es Salaam kuwa moja ya sehemu ya utalii.

  “Wapo wawekezaji wengi kutoka ndani na nje ya nchi ambao wanataka kufungua vituo vya kitalii, lakini wanakosa maeneo, hivyo tumeona ni vema tukazungumza na viongozi wa wilaya za Dar es Salaam ili kuona jinsi tunavyoweza kupata maeneo hayo,” alisema Ole Naiko.

  Alisema wapo wageni kutoka nje ambao wanakuja kufanya kazi za muda mfupi na kuishia Dar es Salaam, huku wakirudi kwao bila kutembelea maeneo ya kitalii kutokana na kukosa muda.

  “Leo tumefanya mashauriano ya ndani, tumejadili mambo mbalimbali ikiwamo kujenga maduka makubwa kila manispaa, ili wageni wanapokuja waweze kununua bidhaa zao,” alisema.

  Alisema maombi ya wawekezaji nchini yamekuwa mengi, lakini wanataka kujua maeneo watakayojengea vituo hivyo na kwamba, sekta ya utalii peke yake ndio yenye uwezo mkubwa wa kuongeza pato la taifa.

  Katika hatua nyingine, Ole Naiko alitaka Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kuharakisha ujenzi wa daraja la Kigamboni litakalo unganisha Dae es Salaam.

  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadiki, alisema Watanzania wengi wamekuwa wakidharau sehemu za kitalii na kuwataka kujenga tabia ya kujifunza tamaduni zao kwa kufanya utalii wa ndani.


  Mimi binafsi nampongeza sana Ole Naiko kwa kuwa maono yake hayo mazuri.Lakini si lazima kusubiri wawekezaji wa nje. Wajibu wa serikali ni nini?
  Ni kweli kuna umhimu sana wa kuwa na maeneo ya kupumzikia,utalii etc walau karibu kila mikoa kama sio majiji yote.
  Leo mtu uko Dar yaani ukishatoka ndani ukiwa huko nje ,hakuna hata sehem za garden or recreations za mtu walau kupumzika baada ya mizunguko.
  Hii ni tataizo la wanamipango wa jiji na wilaya.
  Hivi hawa watu huwa hawaoni nchi zingine wanavyofanya? karibu kila baada ya mita chache kunakuwa na open space like garden etc for resting.
  J ehivi navyo tunahitaji hadi wawekezaji wa kutoka ndani ya nchi/
  Kama kila kitu ni kuwekeza basi kazi ya serikali ni nini hasa?
  Kwanini isiwe ni bora tu kwa hiyo serikali kubinafsishwa pia?
  It is so sad, seeing things which which could have been done by ourself we wait others to do for us.
   
Loading...