Kurutamjanja
JF-Expert Member
- Nov 21, 2013
- 396
- 377
Napongeza uwepo wao Barabarani kwa kulinda usalama wa Vyombo vya usafiri na usalama wa barabarani kwa Ujumla.Lakini Kuna kero kubwa sana tunayopata sisi Madereva Wa Arusha,Vituo ni vingi sana vya kusimamishwa na Polisi hao. Mfano unatoka Monduli, Unakutana na Trafic polisi Uwanja wa ndege,Burka wapo,ujakaa vizuri unawakuta kona ya Mbauda na kote wanakusimamisha,Ngarenaro wapounapita Nairobi road unakutana nao Technical wanakusimamisha, kabla ya Mianzini Mataa unasimamishwa, Na hapo hakuna hata 10km ila unasimamishwa zaidi ya mara tano.kwakeli huu ni usumbufu sana. Na mbaya zaidi wanaposimama hakuna hata sehemu ya kupaki gari ni fujo tu. na vijibarabara vyetu vya Arusha vilivyo vidogo usumbufu unakuwa mkubwa sana.Trafic Polisi Arusha tunaomba mliangalie hilo.