Vituo vya kupiga kura kuongezeka maradufu nchini

Vituo vya kupiga kura kuongezeka maradufu nchini

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
56,943
Reaction score
46,442
lubuva.jpg

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva

Bagamoyo. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema vituo vya kupigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 vitaongezeka mara mbili zaidi ya vile vilivyotumika katika uchaguzi uliopita.

Jaji Lubuva alisema hatua hiyo ni mojawapo ya njia za kukabiliana na changamoto ya Watanzania wengi kutokushiriki katika uchaguzi kutokana na umbali wa vituo.

Alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua mafunzo ya wiki mbili kwa watumishi 20 (15 Bara na watano Zanzibar), mjini Bagamoyo yenye lengo la kuwaongezea uwezo wa kukabiliana na changamoto ambazo hujitokeza nyakati za uchaguzi mkuu. Mchakato wa daftari kwa sasa umefikia kwenye hatua nzuri, tunajiandaa kupata vifaa lakini idadi ya vituo itakuwa zaidi ya 40,000 ukilinganisha na takriban 20,000 vya mwaka 2010. Hii itasaidia kushawishi Watanzania kujitokeza kwenda kupiga kura, alisema Jaji Lubuva na kuongeza:

Changamoto nyingine ni elimu ndogo kwa wapigakura wanaohama eneo moja kwenda jingine bila kufuata utaratibu, matokeo yake wanakosa haki ya kupiga kura.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Salim Jecha Salim alisema imani ndogo ya matokeo miongoni mwa wanasiasa imekuwa ni moja kati ya changamoto kubwa inayowasumbua katika nafasi zao.

Hiyo ni changamoto ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara katika chaguzi, wengi wamekuwa hawana imani kabisa na matokeo tunayokuwa tunatoa katika kipindi cha uchaguzi, hivyo tunachokifanya ni kuwaelimisha Watanzania, alisema Salim.

SOURCE: MWANANCHI APRILI 29, 2014.

My Take.......

Chadema malalamiko yenu yamesikilizwa daftari litaboreshwa na vituo vitaongezwa Uchaguzi Mkuu 2015 nadhani lawama zenu zitakuwa zimeisha hatutaki tena visingizio.
 
Chadema hawatakosa sababu,

Watasema vyumba vya kupigia kura havikuwa na AC...
 
mkuu kama wakifanya hizo itakuwa poa sana ili watu wasisumbuke kwenda kutafuta vituo mbali
 
Muhimu ni kura za uwazi na wingi wa vituo sio hoja.

Wachukue mfano wa uchaguzi uliofanyika Kenya mwaka jana.

Matokeo yawe live. 🐞
 
Muhimu ni kura za uwazi na wingi wa vituo sio hoja.

Wachukue mfano wa uchaguzi uliofanyika Kenya mwaka jana.

Matokeo yawe live. 
Mkuu,

Kura za wazi zinakuaje?
 
Mkuu,

Kura za wazi zinakuaje?

Kura za uwazi : mpiga kura aweze kupiga kura bila ya vitisho, bila ya kuangaliwa ni wapi anatia kura yake hasa hasa wafanyakazi wa serikali.

Wafanyakazi wa serikali hulazimishwa kuitilia CCM na kinyume cha hivyo ni kuachishwa kazi.
 
Mkuu kura ni ya siri nani atajua ummepigia nani!!!
 
Mkuu kura ni ya siri nani atajua ummepigia nani!!!

Kwetu Zenji unafatiliwa kiaina kiasi wanajua kura yako umeweka sehemu gani.

Hii ni kwa sababu CCM si chaguo la Wazanzibari wengi. Na kwa kuthibitisha maneno yangu kila kukiwa na uchaguzi lazima waletwe wapiga kura mamluki kutoka Bara.

Na kama kweli kunakuwa na uchaguzi wa haki na usawa yaani wa UWAZI, CCM Zanzibar haishindi maisha.
 
mzenjiboy

Nadhani hii Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haipo Zanzibar, Zanzibar ipo (ZEC).
 
Last edited by a moderator:
mzenjiboy

Nadhani hii Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haipo Zanzibar, Zanzibar ipo (ZEC).

Kama sikosei wanafanya kazi kwa mahusiano ya karibu sana sidhani kama kila chombo kina sheria tafauti na chombo chengine.

Sina uhakika lakini. 🐬
 
Last edited by a moderator:
Kama ilvyo kwa katiba jambo la uchaguzi mkuu ni nyeti napendekeza ipigwe kura ya wazi, Mtu akifika kwenye kituo atamke wazi mgombea anayemtaka na kura yake ichukuliwe, unashangaa huo si ndo utaratibu ambao ccm wameuasisi ?
Mkuu,

Kura za wazi zinakuaje?
 
My Take.......

Chadema malalamiko yenu yamesikilizwa daftari litaboreshwa na vituo vitaongezwa Uchaguzi Mkuu 2015 nadhani lawana zitakuwa zimeisha.

Kaka siyo CHADEMA kuna mjomba wako huku toka mwaka juzi anataka kupiga KURA sasa kama Daftari litaboreshwa nadhani atafurahi sana.Nitamjulisha baadaye.
 
safi tume tunataka mambo ya ende vizuri
pia ni nafasi kwa vijana wa arusha kupata uwakala kama walivyopelekwa kalenga hakika mboe ataajiri ndugu zake kama kawaida yao maana watu wa arusha ndo wanaowaamini hakika chadema walaghai
 
sasa naona intarahamwe wamekuja na stahili mpya ya wizi
 
Back
Top Bottom