Muundo wa zahanati huwa ni kufanya kazi masaa 8 kwa siku 5 tu kwa wiki, siku za wikiendi na siku kuu ni siku za mapumziko kwa watumishi wake.
Mtumishi wa zahanati asipopumzika jumamosi na jumapili maanayake atafanya kazi mwezi nzima bila kupumzika jambo ambalo halipo
Mtumishi wa zahanati asipofunga kituo cha kazi saa 9 na 30 mchana maana yake anaweza fanya kazi masaa 24 nacho ni kitu kisicho kuwepo.
Mamlaka husika zimezifanya zahanati kuwa ni sehemu ya kutibu wagonjwa wenye matatizo kidogo na ndio maana kunakuwa na watumishi wachache sana pengine hata wanne tu hivyo sio rahisi kupangiana shift ili wafanye kazi masaa 24.
Hatahivyo kwakuzingatia wagonjwa waliokatika hatari ya kupoteza maisha, au kupata ulemavu ikiwa watachelewa kupata huduma, mamlaka husika zimeweka utaratibu wa walau mtu mmoja anashika zamu kwa ajili ya kutoa duma ya kwanza na kuwapa rufaa wagonjwa hao walio katika hari tete. Mtumishi huyo hufanya kazi hiyo akiitwa kutokea nyumbani kwake kwani huwa anakuwa ameweka jina na namba yake ya simu katika mlango wa zahanati.
Mkitaka huduma ya uhakika siku za wikiend na jioni baada ya saa 9 na 30 muende kituo cha afya wanapolaza wagonjwa.