Vituko | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vituko

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by klorokwini, Jun 29, 2010.

 1. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  aahhh vituko hivi vituko, visikieni jamani
  jimama kakosa mwiko ,atumia wa jirani
  keshazua sokomoko,na gumzo mtaani
  hakukitaka kijiko ,alichonacho nyumbani.

  mwengine katuchekesha,vioja katuletea
  usiku kucha kakesha ,jasho limemuenea
  eti mawe achemsha,supu yake aisubiria
  hakika alituchosha ,tukaamua kuishia.

  na hiki kitendawili ,aah jei efu tegueni
  wengi wenye akili,kimewashinda yakini
  kapigwa risasi mbili,bado yupo duniani
  hazimtoshi; halali ,ya tatu aitamani .

  ajabu hii ajabu, kwakweli inashangaza
  haking'ari si dhahabu,kimejaa miujiza
  wengi wanapata tabu,tena kinawaumiza
  wala hakina aibu ,ni wengi kimewakwaza.

  na mwisho hii ajali,hakika yasikitisha
  nahodha leo kafeli,jahazi kalizamisha
  abiria hawakujali ,kuyapoteza maisha
  kisha watoa kauli,nahodha kawaridhisha.


  hehehehe ni mimi malenga wenu klorokwini a.k.a 2pac wa kigamboni.
   
 2. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  hii thread toka june 2010replies-0views-793
   
 3. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  heheh ukiona hivyo ujue hawakuelewa!

  halaf ilikuwaje kuwaje ukaichimbua? khaaaa! nimeshangaa halaf nikasapraizi
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  Lugha ni ngumu kuliko hisabati
   
 5. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  kashairi katamu hako ngoja nikaprinti?hv ukitaka huchukua kitu hadi invisible authorize?
   
 6. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #6
  Nov 25, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  Smile bana! haka kashairi mie mwenyewe nilokaandika sikaelewi halaf wewe unataka kukaprint? khaaa!
  Halaf hapo red huyo jamaa ana authorize ban tu
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Nov 25, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Klorokwini unatisha!
   
 8. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #8
  Nov 25, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Una hamu na talaka eh? Eti nyumbani una kijiko na ww wataka mwiko wa jirani! Mie simoo!
   
 9. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #9
  Nov 26, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  wewe kingast mchokozi sana siku hizi
   
 10. klorokwini

  klorokwini JF-Expert Member

  #10
  Nov 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 8,710
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 135
  heheeh mwalim hii "kutisha" ni ya kusifu au ile ya sura mbaya? kumbuka tuko jukwaa la lugha hapa hatuko chit chat!
   
Loading...