Vituko vya UDOM - Wanafunzi kumwita mhadhiri shemeji!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vituko vya UDOM - Wanafunzi kumwita mhadhiri shemeji!!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Nzi, Feb 27, 2011.

 1. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #1
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,535
  Trophy Points: 280
  Salaam wana JF!

  Sote tunakifahamu chuo chetu kikuu cha Dodoma. Ni chuo ambacho kumekua na vituko vingi vikiripotiwa toka pale. Mfano,wanafunzi kufundishwa na wahadhiri wenye shahada moja! Kuitwa chuo cha kata kutokana na kua na uhaba wa wahadhiri wenye sifa na vigezo! Makamu msaidizi wa mkuu wa chuo kujiita kondoo mweusi,mara kuku anayeatamia! Kuitwa chuo cha chama (CCM). Chuo kutoa shahada ya uzamivu kwa mkwere wakati chuo hakijawahi hata kutoa mwanafunzi 1 wa shahada hiyo n.k.

  Ila hiki kituko cha wanafunzi kuwaita baadhi ya wahadhiri shemeji,mimi kimeniacha hoi.

  Kutokana na chuo kua na wahadhiri wengi vijana,kumetokea tabia ya wahadhiri hao kujisevia wanafunzi wa kike,kiasi kwamba hadi wanafunzi wenzao wanafahamu tabia hizo na mwishowe kuamua kuwaita wahadhiri hao wanaotembea na wanafunzi wenzao wa kike,mashemeji!

  Hakika UDOM kuna vijambo na vituko!
   
 2. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #2
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hiyo ya mashemeji nafikiri ipo kila chuo maana hata maprof nao wamo kwenye kujisevia
   
 3. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #3
  Feb 27, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Natamani na mie niwe lecturer
   
 4. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #4
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Mambo makubwa kwenye vyuo vya kisasa. Maprofesa kuitwa mashemegi hayo ni mapya (made in Tanzania) hata huko Ulaya hakuna.
   
 5. S

  SARAWAT Member

  #5
  Feb 27, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sasa wewe ndugu, university ni adult education, au hujui acha ushamba, kufa kwa kiu ukiwa baharini ni dhambi
   
 6. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #6
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Chuo kikuu ni sehemu ambayo wanafunzi ni watu wazima na wana uhuru wa kujiamulia mtu wa kufanya naye mapenzi hata kama ni mhadhiri. Hiyo inajulikana sehemu zote duniania, ndiyo maana kumekuwa na hadithi nyingi za wanandoa waliojuana huku mmoja akiwa mhadhiri na mwingine akiwa ni mwanafunzi. Tatizo kubwa ni pale kunapokuwa na differential authority baina yao. Kwa mfano kama mhadhiri akiwa anafundisha somo ambalo msichana au mvulana anayefanya naye mapenzi anahudhuria. Kutopkana na conflict of interests, hali hiyo hairuhusiwe na ni kosa kubwa sana ikijulikana kwa uongozi wa chuo. Inapotokea hivyo, inabidi mhadhiri aachie somo hilo lifundishwe na wahadhiri wengine.
   
 7. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #7
  Feb 27, 2011
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Duuh, kweli ngoma haitakwisha!
   
 8. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #8
  Feb 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Duu kama ndo hivo, basi wakuu wakitangaza kazi udom tujuzane :A S 13:
   
 9. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #9
  Feb 27, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Kwa hiyo wanafunzi walitaka wahadhiri wakihitaji kuoa wakatafute machangudoa? Au waende vijijini? Nao hao wasichana wengine si ajabu wakaishia kuolewa na hao mashemeji, sasa kuna ubaya gani hapo?

  Kibaya tu ni kama uhusiano wa mhadhiri na mwanafunzi unahusisha suala la Marks au kama kuna suala la ubakaji. Wale wote ni watu wazima, kama wametongozana na kukubaliana hakuna shida kabisa. Ebu fikiria Mwalimu wa Sociology anatembea na mwanafunzi wa uhandisi baada ya kutongozana vizuri tu, kuna tatizo gani hapo?.

  Au labda wanafunzi wanafikiri Mhadhiri asingechukua mwanafunzi fulani, wao (wanafunzi) wangeweza kumpata huyo demu kirahisi?
   
 10. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #10
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,857
  Likes Received: 4,535
  Trophy Points: 280


  Hoja inakua je ikitokea huyo mhadhiri anajisevia mwanafunzi anaemfundisha,inakuaje hapo? Huoni kama kunaeza tokea conflicting interests kwny masuala ya marking and continuous assessment? Pia huoni kama wanafunzi wengine watahisi ka mwenzao atapendelewa? Tabia hii inaweza sababisha uvujifu wa mitihani hususani pale wanafunzi watakapomshauri mwanafunzi mwenzao wa kike anaeseviwa na mhadhiri,kwenda kumpumbaza mhadhiri(kwa maluvi davi) ili amwonyeshe mtihani.

  Ni kweli ni adult learning na mahusiano yanaruhusiwa ila mazingira ya kutokea kwa conflicting interests yanafanya tabia hii kua haifai. Hii ni sawa na kuchanganya siasa na biashara.
   
 11. M

  Mfwalamanyambi JF-Expert Member

  #11
  Feb 27, 2011
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 434
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  kazaaazi kwelikwli. Na walishatangaza kazi mwisho wa kutuma maombi ni 28 Feb 2011. Mashemeji watongezeka hasa ukichukulia HESLB wanasuasua kuwapa pesa.
   
 12. mluga

  mluga JF-Expert Member

  #12
  Feb 27, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 678
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hawa vijana ni ukosefu wa adabu tu, utamwitaje mtu shemeji wakati huna uhakika na mambo yaliyokuwa yanakwenda nyuma ya kitasa? Ndo maana katika dini ya kiisilamu kumshika ugoni ni lazima fataki ikutwe ndani ya mtutu na uwe na masahahidi watatu wasio na ususiano wowote.
   
 13. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #13
  Feb 28, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Na wala si lazima conflicting interests zitokee. Wote tumesoma vyuoni. Nilipokuwa chuoni niliwahi kushuhudia mwanafunzi akishindwa mtihani kwenye somo analofundisha mume wake. Na mwingine alishindwa somo alilofundisha baba yake. Kwa hiyo kama mhadhiri anafuata maadili ya kazi wala hakuna matatizo yoyote.

  Kwa upande mwingine habari zote kuhusu uhusiano wa mwanafunzi na mhadhiri zinaweza zikawa uzushi tu. Mara nyingi kwenye vyuo, rumours za shemeji shemeji huwa zinaanzishwa na wanafunzi wa kiume. Moja wapo ya sababu huwa ni wivu kwenye marks. Kwa mfano mwanaume akizidiwa marks na msichana, lazima atasingizia tu kuwa yule msichana kagawa mwili. Ila ikitokea mvulana ameongoza mtihani kwenye somo linalofundishwa na mwalimu wa kike, hamna kinachosemwa. Na tatizo linakua zaidi iwapo msichana ni mrembo au hajatulia kitabia au amewatolea nje wanafunzi wa kiume na wakati huo huo anafaulu mtihani. Lazima mhadhiri atafikiriwa kuwa amepewa uroda. Lakini si lazima iwe kweli.
   
 14. n

  nyantella JF-Expert Member

  #14
  Feb 28, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Thanks Nanren you have said it all!
   
 15. M

  Magezi JF-Expert Member

  #15
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Mimi sioni tatizo kama wawili wamekubaliana kuwa na mahusiano yasiyo vunja sheria. Labda niulize, je, ni kosa kwa mhadhiri kuoana na mwanafunzi wa chuo kikuu?? kama siyo kosa basi hapo hakuna tatizo ila tatizo litakuja kama mhadhiri atavujisha mitihani kwa ajiri ya mahusiano ya mapenzi.
   
 16. M

  Magezi JF-Expert Member

  #16
  Feb 28, 2011
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Fanya utafiti kwanza kabla ya kwenda hewani, mambo haya mara nyingi ni wivu wa anafunzi wa kiume.
   
 17. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #17
  Feb 28, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,144
  Trophy Points: 280
  Hii inanikumbusha Binti Mmoja anaejiheshimu wakati anafanya raundi za internship pale Muhimbili, hao madaktari bingwa karibu katika kila raundi walikuwa wakimsumbuwa kutaka ngono na kumwambia "hafaulu" mpaka wamle, ilibidi afike mpaka kwa waziri Meghji (wakati huo), kwani wakuu wa chuo alipowapelekea malalamiko ya kudhalilishwa na kutishwa walimbeza. Meghji akalivalia njuga hilo suala akatia timu mpaka Muhimbili akawaita wakuu na madaktari husika kwa majina akakaa na kuongea nao, haijulikani walicho-ongea, lakini baada ya hicho kikao akasalimika na akawa anaheshimiwa ingawa alibezwa sana lakini. Alimaliza internship ki usalama.

  Nimeongea hayo kuonesha jinsi ngono na udhalilishwaji wa wanafunzi ulivyotapakaa vyuoni, na si vyuoni tu, hata makazini.

  Hapa utaona wanawake wenyewe ndio huwa dhaifu na wengine huendekeza na kuona kuwa hiyo ndio njia ya mkato ya kuuwa ndege watatu kwa jiwe moja, 1) mitihani atafaulu 2) michuzi atapata 3) raha (kama si karaha) za ngono atapata.

  Wenye msimamo kama huyo binti nilie muhadithia hapo juu, huwa si rahisi kuwarubuni.
   
 18. P

  People JF-Expert Member

  #18
  Feb 28, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hufai kwenye jamii ya wasomi
   
 19. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #19
  Feb 28, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..Mhhhh!!:A S 13::A S 13::A S 13::A S 13::A S 13::A S 13:
   
 20. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #20
  Feb 28, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,373
  Likes Received: 3,134
  Trophy Points: 280
  kati ya wanaoitwa shemeji kikwete hayumo kweli?.....maana ni mzee wa totoz kishenzi ndiyo maana ZE UTAMU ILIFUNGIWA
   
Loading...