Vituko vya mwishoni mwa wiki, achana talaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vituko vya mwishoni mwa wiki, achana talaka

Discussion in 'Matangazo madogo' started by kilimasera, Jun 8, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  KATIKA hali ambayo haijazoeleka katika jamii, mwanamke mmoja [jina kapuni] [26] ameshangaza wanafamilia kwa kuchana talaka iliyoandikwa na mume wake mara baada ya kukabidhiwa na mumewe huyo.
  Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo alitumiwa talaka hiyo na mumewe kwa kile kilichodaiwa kuvunja moja ya amri alizopewa na mume huyo wakati wanaingia katika mkataba kabla ya kufunga ndoa yao.

  Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo alitumiwa talaka hiyo na mumewe akiwa mkoani Pwani katika moja ya sherehe za unyago mkoani humo.

  Imedaiwa kuwa, mwanamke huyo aliondoka jijini Dar es Salaam akimuaga mumewe huyo kuwa anaenda kwenye sherehe ya harusi ya moja ya ndugu zake katika ukoo wake kama mbinu ya kuruhusiwa na mume wake.

  Imedaiwa awali mume huyo kabla hajamuoa mwanamke huyo walikubaliana kuwa mkewe asiwe anahudhuria shughuli za ngoma za unyago zinazopendelewa kufanywa mara kwa mara katika familia yao ikiwa ni kuenzi utamaduni endelevu wa kabila hilo. Walioana mwaka mmoja uliopita baada ya kuafikiana masharti hayo.

  Imedaiwa kuwa mwanamke huyo aliweza kuvumilia kutohudhuria shughuli hizo kwa kipindi cha mwaka mmoja na kudaiwa kupata malalamiko kutoka kwa ndugu zake kuwa ametengana na familia kwa kuwa hahudhurii shughuli hizo na ilidaiwa kuwa familia yake ilitishia kumtenga iwapo hatakuwa akihudhuria sherehe hizo.

  Mwanamke huyo alimdanganya mumewe na kumuomba ruhusa kuhudhuria moja ya harusi kumbe alikuwa anakwenda kuhudhuria shughuli hizo za kitamaduni ambazo mume wake huyo alimpiga marufuku.

  Mume huyo alifanya uchunguzi na alibaini kuwa hakukuwa na shughuli ya ndoa bali kulikuwa na shughuli ambayo hapendi mke wake ahudhurie na alimpiga marufuku kuhudhuria.

  Imedaiwa mume huyo alipandwa na jazba na aliandika talaka moja apelekewe mkewe.

  Mkewe alipokabidhiwa talaka hiyo aliichana hadharani na akidai hakuna kosa alilolifanya na aliendelea na shuhguli zake zilizompeleka huko na kudaiwa atarudi nyumbani kwake leo.

  Kitakachoendelea mtafahamishwa
   
 2. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,080
  Likes Received: 7,306
  Trophy Points: 280
  Ndo tabu ya kuoa Mzaramo au ******!!
   
 3. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Huyo jamaa aliingia choo cha kike mwenyewe.
   
 4. Donnie Charlie

  Donnie Charlie JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2011
  Joined: Sep 16, 2009
  Messages: 6,575
  Likes Received: 842
  Trophy Points: 280
  miaka hiyo kabla hawajauza maeneo yao hapa mjini unaweza kukuta ngoma inaanzia tandika mama anapika ikipita tu anaacha kila kitu kama kilivyo na akirudi mume anakuta milango wazi kumbe mke kasindikiza ngoma mbagala, hapo lazima watoto kama watano wapotee.
   
Loading...