Vituko polisi bagamoyo

Nyenyere

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
14,843
Reaction score
10,765
Njemba moja jana ilitinga katika kituo cha polisi Bagamoyo ikiwa na ndoo yenye dawa kama ya babu kuomba ulinzi. Jamaa huyo alidai kuwa ameoteshwa dawa hiyo na kwamba masharti yake ni dawa kulindwa na polisi kwa siku tatu mfululizo ndipo iwe na uwezo wa kuponya. Ilibidi busara itumike kwa polisi kumuelekeza aende hospitali kwani ndio wanaoshughulika na madawa na si polisi.

Mtu mwingine akiondoka kwa jina la amedai kuwa na mahusiano ya kindoto na babu wa loliondo. Mtu huyo ambaye naye ameanza kutoa dawa wa mtindo wa babu anadai huko wanapokutania yeye ni mkubwa ki cheo kwa babu, na kwamba babu analijua hilo. Alipotakiwa kueleza kama wanafahamiana na babu alikataa kuwahi kukutana zaidi ya ndotoni. Hivyo ameitaka serikali kuwapeleka watu kwake mara moja ili wakapate tiba kupunguza msongamano na mateso ya kwenda kwa babu.

My take: No comment.

Source: Wapo
 
Njaaaa kujumlisha tamaaa na kukata tamaa maisha!!!take it
 
Tanzania, watu hawataki kusoma shule wanataka watoke tu kirahisi rahisi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…