Vituko mitandaoni. Tupia chako

Jamaa​

MZEE: sasa huyu mgeni sijui alale wap?
MKE: saa hizi ni usiku sana, akalale tu chumbani kwa Bebi, hakuna namna.

Jamaa alivyoambiwa akawaza labda huyo Bebi pengine ni mtoto mdogo anakojoa kitandani au analia usiku, asije msumbua bure..

JAMAA: wala msipate tabu mi ntalala hapa hapa kwenye kochi..
Akalala, asubuhi wanakunywa chai akaibuka mrembo matata Sana..,

BINTI: Naitwa BEBI, we mwenzangu waitwa nani?
Jamaa akapigwa bumbuwazi, almanusra ajimwagie chai..
Kwa unyonge na majuto akajibu tu, mimi naitwa Fala 😭
 

Mama​

Kuna mkaka alitembelewa na mama yake mzazi.
Wakiwa sebuleni yeye, mama na mke wake, mke wake akaanza kuonekana tofauti kama vile anajiskia vibaya.
Akaenda chumbani. Baada ya muda mfupi yule mkaka akamfuata.

Wakakaa sana huko kisha mkaka akarudi sebuleni kuendelea kuongea na mama yake. Lakini zipu ya suruali yake ilikuwa wazi. Mama akamuuliza, mkeo anaendeleaje? Akamuambia, anajisikia vzr sasa. Nimempa panadol.

Mama akatabasamu na kumwambia mwanaye, sawa. Lakini siku nyingine ukishatoa panadol ukumbuke kufunga pharmacy😊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…