K
Zuzu kaniuliza, “Anko, unajua vitu vinavyoanzia na K ni vitamu sana.”
Nikashtuka, “Astaghafilulah we mtoto! Niondolee uchuro wako hapa!”
Zuzu akatabasamu. Akaendelea kuongea kabla sijafanikiwa kumzuia.. “Kweli kabisa anko. Vitu vinavyoanza na K ni vitamu sana kwa mfano kuku, kalimati, keki, kabab, katleti, kashata, kisheti, karanga, korosho na karoti.”
Nikashusha pumzi. “Ahaa! Kumbe ndo hivyo, ni kweli!”
Zuzu akanitupia swali. “Kwani we anko ulidhani nini?”