Vituko mitandaoni. Tupia chako

Kumbe alimuahid kuwa ata mniniliii shemela
 
Wengine sio wezi, mie simu yangu nishaisahau sehemu tofauti tofauti mara 4 na naipata kwa kuipiga.
Mi mwenyewe simu ilicholopoka kwenye daladala pale makumbusho na nilikuwa wa mwisho kushuka kumbe akaikota konda.
Nimefika huku juu jirani na CHAUMA ndio najikuta sina simu, nikakata tamaa kabisa.

Baada ya kufika kinondoni nikasema nijaribu tu kuipigia nikaona inaita kweli na ikapokelewa.
Baada ya mazungumzo jamaa akasema yeye ni konda ameikota kwenye siti ya daladala so kama vipi niende segerea akanipe.

Nikamuuliza si utarudi makumbusho? akasema atarudi ila mpaka zamu ya kupakia ifike.
Yule jamaa nilirudi kumsubiria Makumbusho na bahati nilibaki na kitiketi chenye namba ya gari, kwa hiyo gari ilipofika tu nikamfata na akanipa.
 
Watu wema bado wapo aisee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…